Monday, 21 March 2011

MAJONZI MAKUBWA TANZANIA!!!!!!! KUNDI LA TAARABU LA FIVE STARS LAPATA AJALI USIKU HUU, ZAIDI YA WATU 10 WAHOFIWA KUFA!!!

Hawa ndo baadhi ya wanamziki wa Five Star Modern Taarab
WANAMUZIKI WA BENDI YA FIVE STAR MODERN TAARABU ZAID YA 10, WAMEPOTEZA MAISHA KWA AJALI YA GARI HUKO MOROGORO ENEO LA MIKUMI NA WENGINE KUJERUHIWA VIBAYA SANA NA HALI ZAO NI MBAYA. GARI HILO LILIKUWA NA WATU 22, LAKINI WAMENUSURIKA 5, HUKU WATATU WAKIWA WAMEUMIA KIDOGO. KWA MUJIBU WA VYANZO VYA HABARI INADAIWA GARI HILO LILIKUWA KWENYE MWENDO MKALI NA KUPELEKEA KUGONGA LORI LILILOKUWA LIMEPAKIA MBAO PEMBENI YA BARABARA, KUGONGA HUKO ILIPELEKEA VIFO VYA WATU 8, HAPO HAPO NA KISH AKAENDA UPANDE WA PILI AMBAPO LORI LINGINE LILIKUWA LINATEMBEA NDIPO ILIPOISHIA NA KUSABABISHA VIFO HIVYO ZAIDI YA 10, NA MAJERUHI WENGI.MAITI ZIMEHAARIBIKA VIBAYA SANA HALI AMBAYO HAZITAMBULIKI KUTOKANA KUWA VIWILI WILI. 

Habari kwa hisani ya Andrew Chale (Tanzania Daima)

Kwa picha na habari zaidi juu ya ajali hii bofya hapa Globalpublishers

Majina ya wanamuziki wa bendi ya Five Star Modern Taarab waliokufa katika ajali ya gari Mikumi mkoani Morogoro usiku wa kuamkia leo yamefahamika.
Kwa mujibu wa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Morogoro Be. Ibrahim Mwamakula, marehemu hao ni Issa Kijoti, Nasoro Madenge, Mapande, Fembe Juma, Omary Hashim, Tizo ,Omari Tall,Ngeleza Hasan,Hamisa Omari,Maimuna , Haji Msaniwa na mcheza show wa kundi la Kitu Tigo Ilala

“ Hii ajali imepoteza watu 13 kati ya hao 12 wamefariki papo hapo na mmoja
amefariki akiwa anapatiwa matibabu Hospitalini.

"Ni ajali mbaya kutokea iliyohusisha magari matatu, ambapo waliokufa wote ni kutoka kwenye basi dogo la wasanii wa kikundi cha Five Stars na kusababisha majeruhu tisa kulazwa” alisema Mwamakula, akifafanua kuwa kati ya waliokufa 10 ni wanaume na watatu ni wanawake.

Amesema majeruhi tisa ambao wote ni wasanii waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Morogoro ni pamoja na Mwanahawaa Ally( 55) kutoka Kundi la East African
Melody, ambaye alikuwa ni msanii mwalikwa, Susana Benedict(32), Zena Mohamed
(27), Samila Rajab (22)na Mwanahawa Hamisi (36)ambao wamelazwa wodi namba
tatu.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliwataja
wasanii wengine waliolazwa katika Hospitali hiyo ni pamoja na Ally Juma
(25), Rajabu Kondo ( 25), Issa Hamis , Shaaban Hamis (41) na Msafiri Musa
(22). 

Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, kuwa dereva huyo aliligonga lori hiyo wakati akijaribu kulikwepa Lori jingine lililokuwa likotokea mbele yake lenye namba T 530 BHY lenye tela T 182 BKB aina ya Scania ambapo katika harakati hizo basi hilo lililigonga Lori hiyo mbele pembezoni na kusababisha magari hayo kuanguka.

Alisema kuwa baada ya kuliparamia Lori hiyo , basi hilo liliyumba na kuhama uoande wake na kujibamiza kwenye Lori lililokuwa mbele yake ambalo halikuwa na mzingo kitendo kilichofanya paa la basi hilo kukatwa wa juu ambapo watu 12 waliokuwa ndani ya basi ndogo hilo kufariki dunia papo hapo na wengine saba kujeruhiwa vibaya .

Hata hivyo alisema , majeruhiwa mmoja kati ya saba alifariki dunia wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro alipofikishwa kutoka eneo la tukio na kutambuliwa na ndugu zake kuwa ni Haji Mzaniwa ( 38), mwimbaji wa kikundi hicho.

Stay connected with Jestina-George.com, follow us on Twitter and Facebook for all the latest fashion trends, latest celebrity news, gossip, showbiz & current affairs

1 comments/maoni:

Anonymous said...

Jamani! Mungu awalaze mahali pema peponi!

Post a Comment

Toa maoni yako kwa uhuru na tafadhali naomba usichafue hali ya hewa humu ndani wala kujeruhi hisia za mtu au watu. (Let's please maintain a high level of discipline! Zero tolerance policy on abussive language!) Asante na karibu sana.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Mixed Posts