MTOTO HUSSEIN RISASI ANATAFUTWA...!!!

Familia ya Bw Alhaj Abdul Risasi wa Kawe jijini Dar es Salaam inatangaza kupotelewa na mtoto wao Hussein Risasi (15) anayesoma shule ya Msingi Olympio iliyopo Upanga Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Alhaj Risasi ni kwamba Hussein alitoweka nyumbani kwao Kawe jijini Dar es Salaam Ocktoba 25 mwaka huu mara baada ya kurejea akitokea shuleni.
Kabla ya tukio hilo Hussein alianza utoro wa kwenda shule kwa madai kwamba amekuwa haelewi anachofundishwa na walimu wake na kwamba wanafunzi wenzake wamekuwa wakimcheka  kitendo ambacho hakukipenda.
Akifafanua  zaidi Alhaj Risasi amesema kuwa, kutokana na tabia hiyo ya utoro aliyoianza Hussein ambaye ni pacha na Hassan Risasi anayesoma Nairobi, alimwita na kumkanya kutokana na vitendo hivyo.
Hussein amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya athma tangu utoto wake jambo linaloathiri pia afya yake mara kwa mara.
Kwa yeyote atakayemuona anaombwa kutoa taarifa kituo chochote cha Polisi nchini au kupitia namba za simu 0715  611 277, 0713  314  442  au 0787 377 822.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment