SIKILIZA KITU KIPYA CHA LADY JAY DEE 'YEYE'...!!!

---
Mume wa Lady Jaydee Gardner G Habash jana ameitambulisha single mpya ya Jide ndani ya Clouds FM 'The People's Station'. Single hiyo iitwayo ‘YEYE’ ndo  inakua single yake ya kwanza kuitoa mwaka huu.
Kazi imefanywa na Producer Lamar ambapo Gardner amesema Jide ameimba kama Lugha nne tofauti ndani ya hiyo single, kiingereza, kiswahili, Kilingala na kama kizulu na kiganda.
Amesema “hii ndio ingekua single yake ya kwanza kwenye album yake mpya ya The Best of lady Jaydee kama utakumbuka mwaka jana ndio walitoa single ya kwanza ya ‘WANGU’ lakini hii single ndio ilitakiwa kuwa ya kwanza baadae ilipokuja ‘WANGU’ akasema sijawahi kufanya wimbo ambao nimeandikiwa na mtu mwingine kwa hiyo acha ‘WANGU’ ndio utoke wa kwanza”
Kwa mujibu wa Gardner, Baada ya Oliver Mtukudzi kuja na kufanya kolabo, Jide alisema kwa sababu habari ya Mtukudzi ilikua ya kusisimua ilibidi waisitishe hii single ili kolabo ya Mtukudzi itoke lakini sasa ndio ameitoa hii single ambayo ameichelewesha kuitoa toka january kwa sababu yuko Afrika kusini kujifunza kupiga Piano hivyo aliona haitakua na manufaa wakati yeye hayupo anaweza kuulizwa maswali asiweze kujibu. Source: Millardayo.com
KWANGU MIMI HUU NDO WIMBO WANGU NO 1 KWA SASA NAUPENDAJE, NA NINA UPLAY NON-STOP!!! I'M SURE YOU'RE GONNA ENJOY IT TOO! BIG UP MY JIDE KEEP  DOING YOUR THING & GOD BLESS.
MUCH LOVE
JG
XOXOX
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment