BREAKING NEWS!!!! MELI YA ABIRIA INASEMEKANA KUZAMA ENEO LA CHUMBE VISIWANI ZANZIBAR...!!!...!!!

Inasemekana boat yenyewe iliyozama ndo hii
---
Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba Meli ya MV Seagull iliyokuwaikielekea Zanzibar ikiwa na abiria 200 imezama katika kisiwa cha Chumbe. Meli hyo ilitoka Dar Es Salaam leo saa 7 mchana. Jitihada za uokoaji zinaendelea.

Tutazidi kuwaletea habari kadri tunavyo zipokea.

Update:
Meli iliyo zama ni MV Seagull ilikuwa na idadi ya watu 250 na mpaka sasa huduma ya uokoaji inaendela.

Askari wanaokoa wananchi kwa kutumia boti hizi - among others...
Update:
Mpaka sasa maiti 12 zimepatikana wakiwemo watoto wa 3. Hali ya hewa ni mbaya sana, upepo ni mkali sana. Tuendelee kuwaombea hawa ndugu zetu pamoja na wanao saidia uokoaji ili watoke salama na bahari iwezee kutulia.

Juhudhi za uokoaji bado zinaendela

Serikali yaongeza wazamiaji kutoka Kikosi cha KMKM pamoja na Jeshi kuendelea kuokoa raia waliokumbwa na mkasa wa kuzama meli, Mungu aendelee kutenda miujiza yake kuweza kuokoa walio hai.
Baadhi ya abairia waliookolewa kutoka kwenye meli iliyo zama mapema leo
 Moja kati ya maiti zilizopatikana baada ya kuzama kwa meli ya MV Skagit
Majeruhi alieokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.
Wananchi mbalimbali wakishuhudia tukio la kuokolewa watu waliozama na meli ya Star Gate huko katika hukokatika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Majeruhi wakipatiwa Mablanketi kwa ajili ya kujihifadhi baada ya kuokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

 Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Amer Kificho pamoja na mawaziri mbalimbali wakiwa katika Eneo la Bandari wakishuhudia kuletwa kwa majeruhi mbalimbali waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akiwa katika Eneo la Bandari akishuhudia kuletwa kwa majeruhi mbalimbali waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akiwa na Viongozi Wakuu wa Serikali alipofika katika Ofisi za Shirika la Bandari, Malindi Unguja kupata taarifa sahihi ya ajali ya kuzama kwa Meli ya MV Sky Get ikitokea Dar es Salaam kuelekea Unguja.
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na kuzama kwa Meli ya Star Gate hukokatika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Update kutoka TVZ 
Mpaka sasa maiti 25 na waliokolewa ni 124 wengi wawaliokufa ni wanawake na watoto.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment