KASEBA VS CHEKA NANI ZAIDI UWANJA WA TAIFA KESHO...!!!


Bondia Japhet Kaseba kushoto na Francis Cheka wakionyeshana umwamba wa kila mmoja kutaka kumchakaza mwezake wakati walipopima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika katika uwanja wa taifa siku ya jumamosi katikati ni mratibu wa mpambano huo Kaike Siraju.

Baadhi ya Mabondia na Makocha wakisubiri kupima uzito kwa mabondia kwa ajili ya Mpambano wa siku ya sabasaba katika tamasha la matumaini.
Bondia Francis Cheka akipima uzito kwa ajili ya kumkabili mpizani wake Japhet Kaseba kesho katika uwanja wa Taifa wakati wa Tamasha la matumaini ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali mbali 
Mratibu wa mpambano wa ngumi Kaike Siraju katikati akiwainua mikono juu mabondia Japhet Kaseba kushoto na Francis Cheka baada ya kumaliza kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya sabasaba katika uwanja wa taifa wakati wa Tamasha la Matumaini kwa watanzania litakalokusanya burudani mbali mbali.
Bondia kutoka Kambi ya Ilala Ibrahimu Class akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Sadiki Momba utakaofanyika Kesho katika uwanja wa Taifa
 Bondia toka kambi ya Ilala Ibrahimu Class akipima Afya kwa ajili ya mpambano wake na Sadiki Momba utakaofanyika kesho katika uwanja wa taifa
 
Bondia Francis Cheka akipima Afya kwa ajili ya mpambano wake na Japhert Kaseba utakaofanyika kjesho katika uwanja wa Taifa. 
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment