MAHOJIANO RASMI JUU YA TAMASHA LA WAJANJA WA VODACOM-MWAMBAO FM HAPO JANA...!!!

Pichani shoto ni Meneja wa mahusiano wa Vodacom Tanzanzania Bw.Matina Nkurlu akimtambulisha Mkuu wa Mauzo wa Vodacom kanda ya Pwani,Bw.Tilio Lupala pichani kulia kwa Mtangazaji wa redio ya Mwambao FM,Kikwato Jr mara baada ya kuwasili kwenye makao makuu ya ofisi hizo jioni ya leo kwa ajili ya kufanya mahojiano ya tamasha la Wajanja wa Vodacom litakalofanyika kesho kwenye Uwanja wa Mpira wa Mkwakwani mjini Tanga.Anaeshuhudia wa pilia kulia ni Afisa Udhamini na Matukio Ibrahim Kaude.
Mkuu wa Mauzo wa Vodacom kanda ya Pwani,Bw.Tilio Lupala pichani kushoto akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa kituo cha redio ya Mwambao FM.Wanaoshuhudia ni Meneja wa mahusiano wa Vodacom Tanzanzania Bw.Matina Nkurlu pamoja na Mtangazaji wa redio ya Mwambao FM,Kikwato Jr.
Mtangazaji wa redio ya Mwambao FM,Kikwato Jr akifafanua jambo mbele ya baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom,kuhusiana na namna mitambo ya kituo hicho kinavyorusha matangazo yake. Anaeshuhudia wa pili kushoto ni Afisa Udhamini na Matukio Ibrahim Kaude.
Pichani kati ni Afisa Udhamini na Matukio Ibrahim Kaude akifafanua jambo kwa ufasaha wakati wa mahojiano mafupi juu ya tamasha la Wajanja wa Vodacom.
Pichani kulia ni Meneja wa mahusiano wa Vodacom Tanzanzania Bw.Matina Nkurlu akitoa ufafanuzi mbalimbali kuhusiana na mambo mbalimbali yatakayojiri kesho ndani ya uwanja wa Mkwakwani,ambako tamasha la wajanja wa Vodacom litarindima.

Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment