PACHA GREAT AIBUKA KINARA WA SHINDANO LA KUMSAKA MKALI WA SERENGETI FIESTA MC SHUJAA 2012...!!!

 Mratibu na jaji wa shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa 2012,Reuben Ndege a.k.a Ncha Kali kutoka Clouds FM,akimpa maelekezo mafupi Pacha Great mara baada ya kuibuka kinara wa shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa,kwa kuwashinda mahasimu wenzake wapatao 32 waliofika kushirika mchakato wa shindano hilo.shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa limeandaliwa na Prime Time Promotions/Clouds FM kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.
 Wasanii chipukizi walioshiriki shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa,kutoka kulia ni Pacha Great akimchana live kwa kughani msanii mwenzie aitwaye Chalz Gibson wakati wa shindano hilo,ambpo Pacha aliibuka mshindi na kuwa mshindi wa shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa 2012 ndani ya jiji la Arusha.
Mmoja wa majaji wa shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa,Reuben Ndege a.k.a Ncha Kali akifafanua jambo kwa washabiki na watazamaji mbalimbali waliofika kwenye shindano hilo ndani ya ukumbi wa Mawingu Club,mjini Arusha mapema leo jioni.
Majaji wa shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa wakijadiliana jambo,kutoka kulia ni JCB,Reuben Ndege a.k.a Ncha Kali kutoka Clouds FM pamoja na Mdau wa muziki wa hip hop,Mo-Plus.
 Washabiki wakishangilia jambo ukumbini humo.
 Mwanadada mwingine aliyejitokeza kunogesha shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa,aliyejulikana kwa jina la Catrina akiimba kwa sauti tamu kabisa na yenye kusisimua mashabiki jioni ya leo ndani ya Mawingu Club,jijini Arusha.
Msanii mahiri wa hip hop kwa jiji la Arusha atambulikae kwa jina la kisanii,JCB akiwarusha washabiki wa muziki wa hip hop,jioni ya leo ndani ya ukumbi wa Mawingu Club,wakati wa kumsaka kinara wa shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa.
Mratibu wa shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa,Adam Mchiomvu akitajana majina yaliyoingia fainali kwenye shindano hilo,ambalo limekuwa na msisimko mkubwa kwa vijana wengi wa jiji la Arusha,katika mchakato mzima wa shindano hilo walijitokeza vijana 32,wakachunjwa na kupatikana wengine 12,na hatimaye kuwapata sita ambao walishindana vikali,aidha katika sita hao aliihitajika kinara mmoja tu wa kughani kwa miondoko huru.
Mwanadada machachari kabisa aitwaye Tiger Eyes akionesha umahiri wake wa kughani mbele mashabiki waliofika kwenye shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa
Mashabiki wa muziki wa hip hop wakiwa wamekusanyika ndani ya Mawingu Club,jioni ya leo wakishuhudia shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa ndani ya jiji la Arusha,ambapo mshindi katika shindano hilo atabahatika kurekodi albamu nzima ya nyimbo zake,kama vile haitoshi atashiriki kwenye kilele cha jukwaa la Serengeti Fiesta 2012,litakalofanyika jijini Dar.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment