SIKILIZA MAMBO YALIYO TOKEA BAADA YA MAZISHI YA MAREHEMU DOMITIAN RUTAKYAMIRWA MTANZANIA ALIYEFIA NCHINI MAREKANI...!!!

Funzo kwa watanzania wanaoishi nje na ndani ya Tanzania...

Marehemu Domi enzi za uhai wake! R.I.P
---
Ni rekodi kutoka kwenye kipindi cha "Weekend Special" cha redio WAPO FM kuhusu yaliyotokea baada ya msiba wa Domi ambapo familia ya marehemu ilirusha madai kuhusu mali na fedha na kuweka zuio kwamba mke asiruhusiwe kusafiri kutoka Tanzania kurudi Marekani waliko watoto wake. Mtangazaji wa WAPO Radio, Anthony, alizungumza na kila upande unaohusika na suala hili na kisha kuzikutanisha pamoja ili kuwekana sawa kuhusu tuhuma zilizotamkwa. 

"Hizi ni changamoto za maisha ya ndoa, ughaibuni, familia na tamaduni mbili zilizo mbalimbali!"-Subi


Asante sana Subi kwa kushare jambo hili nami kwa kweli ni changamoto na binafsi nimejifunza mengi sana. Inasikitisha sana. Mungu atusaidie na atuepushe na mambo kama haya. 


Taarifa hii ni kwa hisani ya  Subi wa wavuti.com.

‘Plan your future today’ with WESTADI
Join now through www.nssf.or.tz
or 
CLICK HERE


Share on Google Plus

About Jestina George

  Blogger Comment
  Facebook Comment

11 comments/maoni:

 1. Yaaani Hii ni fundisho kubwa sana.Pumzika kwa Amani Domi.Mungu aendelee kuwapa nguvu na Amani familia hizi mbili.Amina.
  .Asante dada Jestina kwa kutushirikisha kusikiliza hili tukio.Ubarikiwe katika KAZI yako Hii kubwa.Amina.

  ReplyDelete
 2. mimi naomba tuwe tunakumbuka kuleta mapadre wawa ungamishe,watubu dhambi.ndio furaha yangu..nasikitika kweli kusikia vitu hivi kama wakristu hawapo vile.

  ReplyDelete
 3. huyu dada amesema hapiki majiko ya gesi stoo yamefuata nini kama sio ya marehem,mafriji yote hayo yanini mimi nadhaniwaelewane tu yaishe.

  ReplyDelete
 4. inasikitisha sana, inaonyesha ni kiasi gani watu hatuna mapenzi. tunaoa na kuolewa kwa sababu tunazozijua sisi wenyewe na si kwa mapenzi. wote tutakufa lakini iwe kwa mapenzi ya mungu na si kwa mwanadamu mwingine kuamua.

  ReplyDelete
 5. Marehemu kwa bahati mbaya hajazaa na mkewe ambaye yupo huku Marekani. Marehemu ameacha mtoto mmoja ambaye alimzaa huko Tanzania, mtoto huyo alikuwa anahudumiwa kila kitu na baba yake. Naona ni muhimu kuongea kuhusu mali za marehemu, je huyo mtoto wa marehemu ambaye tumesikia yupo Tanzania, anapata nini?

  ReplyDelete
 6. Kitu cha muhimu ni kwa familia hizi kukaa pamoja na kujadiliana, siamini wanadamu wenye utashi wanaweza kushindwa kuelewana katika masuala kama haya wamrudie mwenyezi Mungu awape nguvu ya kuweza kukabiliana na changamoto iliyopo mbele yao,pia wakumbuke kuwa MAPENZI YA MUNGU NI LAZIMA YATIMIZWE
  Acheni malumbano na kuchafuana hailipi!
  Tuliopo ughaibuni hata mliopo nyumbani kuna cha kujifunza hapa!

  ReplyDelete
 7. Naomba tukumbuke mahubiri ya Mch. Ferdinand Shideko kwenye ibada ya kumuaga mpendwa wetu Domitian Rutakyamirwa iliyofanyika Jumatano Juni 27, 2012. Mch. Ferdinand Shideko ametueleza jinsi alivyomjua Domi na pia mambo ambayo Domi ameyafanya na kuyatamka wakati anaumwa. Domi aliwasamehe wote waliomkosea na yeye pia aliomba msamaha kwa wote aliowakosea. Ni vyema familia ya marehemu na familia ya mke wa marehemu wakae pamoja na kusameheana kwa yote yaliyotokea. Hili ni fundisho ambalo Domi ametuachia, ya kwamba tusameheane ili twende tukiwa safi kwenye makao yetu ya milele.

  Si vyema kuendeleza haya mambo kwa kwenda kukanusha kwenye vyombo vya habari iwe hapa Marekani au Tanzania, kwani kama kuna ukweli umesemwa au uongo umesemwa yote yanajulikana kwa wote tuliopo hapa Marekani, waliopo Tanzania na MWENYEZI MUNGU pia.

  ReplyDelete
 8. Mimi naona huyu dada wa Domi ndio mtata

  ReplyDelete
 9. Hapa tunachokiangalia mpaka sasa hivi ni haki ya mtoto wa marehemu Domi aliyepo Tanzania ameambulia nini kutoka kwa Baba yake, ni haki kwa Ndugu kuulizia mali ya ndugu yao kwani watoto waliopo marekani tunajua si watoto wa marehemu. Mtoto wa Domi amepata nini?

  ReplyDelete
 10. nafikiri familia ya Domi haikutumia busara katika kudai mali.Ilikuwa mapema sana kuanza kudai mali.maisha ya ughaibuni yanajulikana yalivyo magumu.Wangeacha mke wa domi amlaze mumewe kwenye nyumba yake ya milele kwanza kisha waanze kufuatilia mali.Mama huyu namjua ni mstaarabu.Amemuuguza domi kwa mwaka mmoja na nusu bila msaada wa kipesa kutoka kwa familia ya marehemu. Sasa yaweza kukosa vyote. Time factor and how to express your feelings matters!

  ReplyDelete
 11. Hii habari inasikitisha sana, hapa kilichotakiwa kuangaliwa ni mtoto wa marehemu ambaye msaada mkubwa ulikuwa ni kwa baba yake na wazazi wa marehemu walikuwa na haki ya kudai kwani huyo hakuwa mke wake halali bali ni wa makaratasi tu, na huyo mwanamke kwa nini hakumpa kitu chochote mtoto wa marehemu na huku anajua ana haki. hiyo ni dhuruma na lazima atalipa.

  ReplyDelete