TUME YA UTUMISHI WA BUNGE YATEMBELEA BUNGE LA UINGEREZA.

Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola duniani, Sir Alan Haselhurst(kati) akiwa katika mazungumzo na Mhe.Job Ndugai, Naibu Spika wa Tanzania na Katibu wa Bunge, Dr Thomas Kashililah kwenye Bunge la Uingereza.Naibu Spika anaongoza wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge kwa ziara maalum ya kibunge nchini humo.Mwingine pichani ni Katibu wa CPA Uingereza, Nd.Andrew Tuggey.
Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge wakipata maelezo kuhusu Bunge la Uingereza wakati wa ziara yao.Ziara hiyo inaendelea ikiwa na lengo la kuwaongezea uwezo wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge namna Bunge la Uingereza linavyofanya kazi.  
Naibu Spika akipokea zawadi toka kwa Mwenyekiti wa CPA duniani, Sir Alan Haslehurst walipokutana nchini Uingereza.
Katibu wa Bunge ambae pia ni Katibu wa CPA Afrika, Dr Thomas Kashililah akikabidhi zawadi kwa Katibu wa CPA Uingereza; Nd.Andrew Tuggey wakati wa ziara hiyo.
Picha zote na Saidi Yakubu.

Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment