DUA YA DIAMOND PLATNUMZ KWA MASHABIKI WAKE.

"Ni siku nyingine tena napenda kumshukuru mwenyezi 
Mungu mwingi wa rehema zake kwa sisi wanadamu......
sote kwa ujumla,wewe unaesoma ujumbe huu na ata
 ambae yupo miangaikoni mungu amfanyie wepesi......Binafsi 
Mi mzima kabisa wa afya tele pamoja na 
Familia yangu nzima kwa ujumla.....Namshukuru 
sana Mungu kwa Pumzi yake ya bure 
kwetu na kuzidi kunibariki na kunifungulia milango ya 
Baraka kwenye kazi yangu ya Muziki ....Si kama sisi tuliopo
 hapa wazima ni wema sana machoni pakee lakini kwa 
kudra zake mwenyezi Mungu Tu angali wazima wa Afya....!!
Nachukua nafasi hii kuwashukuru Mashabiki zangu kote 
Nchini na hata nje ya nchi na Dunia nzima kwa support
 yenu kwangu na mapenzi yenu kwangu ya dhati.....!!
Hakuna Nyota Bila Shabiki Bila Nyinyi mi si chochote.....!!
Binafsi Nafurahi sana kuwa karibu na nyie 
japokuwa sio wote ntakaowaridhisha kwa ujumla 
kwa kuwa ni mashabiki wengi sana kila kona na pembe ya Dunia.....
Lakini Mda huu mdogo naopata nafurahi kuwajulia hali kwa pamoja.....

Cha Msingi napenda kuwatakia mafanikio na baraka tele 
juu yenu iwe kwenye masomo, Biashara,kazi hata kwa wale wagonjwa,wasiojiweza na vilema 
Mkono wa Mungu
 ukawe Juu yenu kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwingi wa
 baraka na daima utuwazia Mema Juu yetu hata 
kwa mabaya mengi tumkoseayo...!!
Upendo na Amani daima utawale kati yenu katika Maendeleo 
ya kujenga taifa letu kwa nguvu na umoja kama Nguzo ya 
Muunganiko na umoja kati yetu.....Dini wala ukabila usiruhusu 
vitawale kati yenu na kujenga chuki mioyoni
 mwenu kutokana na tamaa za baadhi ya watu 
kusababisha mtafaruku kati yetu 
viumbe wa Mungu....!!
Mshukuru Mungu kwa hapo ulipo.....Hakuna kitu 
kibaya kama kutokuamini wewe si
 chochote wala si lolote.....
Amini ya kwamba upo dunia kwa makusudi ya 
mwenyezi mungu na Mungu anakusudi na 
wewe hapo ulipo......!!!
Napenda kuwatakia Jioni Njema.....Ni Hayo Tu
    kwa Leo....NAWAPENDA SANA......................................!!!!!!!"
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment