BABU TALE AELEZEA CHANZO CHA KIFO CHA KAKA YAKE ABDU BONGE. ( Audio)

Abdu Bonge aliekuwa Meneja aliekuwa akiongoza Kundi la Muziki la Tiptop Connection akisaidia na Mdogo wake Babu Tale alifariki Dunia jana Jioni, Taarifa za Mwanzo hazikuweza kueleza kuhusu chanzo cha kifo chake lakini leo Mdogo wake Babu Tale ameelezea Jinsi ambavyo kaka yake alipoteza Maisha.


‘Kuna mshkaji wetu mmoja alikua anagombana na mke wake jirani yetu, wakamfata hapa Abdul aende… mara ya kwanza na ya pili akakataa, mara ya tatu akasema ngoja aende’

‘Alivyoenda ukapita ukimya kidogo, baadae kuna mtu akaja kumuita kaka yetu mkubwa mwingine na kumwambia nenda kamsaidie kaka yako mkubwa amedondoka, kaka yangu baadae akanipigia simu akasema Bonge kama amezimia lakini sidhani kama atapona sababu wakati wa kuamulia ugomvi alianguka baada ya kusukumwa nafikiria aliangukia kichogo, kumpeleka Hospitali Manzese wakasema ameshafariki‘ alisema  Babu Tale.Audio clip kwa hisani ya http://millardayo.com
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment