DKT. SHEIN AFUNGUA HOSPITALI YA GLOBAL, VUGA MJINI UNGUJA LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky Salim Hassan Turky wakati alipofika kufungua Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kufungua Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo (wa pili kulia) Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky Salim Hassan Turky.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana mkono wa pongezi na Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky Salim Hassan Turky baada kuifungua Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kuifungua Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo (kushoto ni Dkt,K.Ravindranath Daktari Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Hospital (kulia) Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky Salim Hassan Turky.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo alipotembelea mashine ya Xray baada ya kuifungua Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo (wa kwanza kulia) Dkt,K.Ravindranath Daktari Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Hospital.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Daktari Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Hospital Dkt,K.Ravindranath(wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky Salim Hassan Turky wakiangalia mashine ya kufanyia Upasuaji wakati alipotembelea Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo baada ya kuifungua rasmi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Daktari Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Hospital Dkt,K.Ravindranath (kulia) wakati alipotembelea sehemu mbali mbali za kutoa huduma katika Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo baada ya kuifungua rasmi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mwakilishi wa Mwakilishi wa Kampuni ya Global Hospital ya India Dkt.Nagesh Rao (kulia) wakati alipotembelea katika vyumba vya upasuaji vyenye mashine za kisasa baada ya kuifungua Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo (katikati) Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky Salim Hassan Turky.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Daktari Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Hospital ya India Dkt,K.Ravindranath (katikati) wakati alipotembelea chumba cha wagonjwa mahututi (Theatre) baada ya kuifungua Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo (kulia) Mkurugenzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Dk.Jamala A.Taibu.
Baadhi ya Madaktar na waalikwa katika sherehe ya ufunguzi wa Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Hospitali hiyo leo.
Baadhi ya waalikwa mbali mbali katika sherehe ya ufunguzi wa Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Hospitali hiyo leo.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky Salim Hassan Turky akitoa salamu zake mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) baada kuifungua Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo.
Kaimu Waziri wa Fedha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini akisema machache na kumkaribisha mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) kuzungumza na wananchi baada ya kuifungua Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo inayomilikiwa na Kampuni ya Vigor Turky ya hapa Zanzibar ambayo itatoa huduma za Maradhi mbali mbali.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na taasisi mbali mbali na waalikwa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za ufunguzi wa Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo inayomilikiwa na Kampuni ya Vigor Turky ya hapa Zanzibar ambayo itatoa huduma za Maradhi mbali mbali.

Na Said Ameir, Zanzibar                                                       
28 Machi, 2015
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza kuwa Zanzibar kama zilivyo nchi nyingine inatambua sekta za Afya na Elimu kuwa ndizo msingi wa maendeleo na ukuaji wa sekta nyingine za kiuchumi na kijamii ndio maana wakati wote imekuwa ikichukuwa hatua mbalimbali za kuziimarisha sekta hizo.
Dk. Shein amesema hayo leo mara baada ya kuzindua rasmi hospitali mpya na ya kisasa ya TASAKHTAA iliyopo Vuga mjini Unguja ambayo imejengwa kwa ushirikiano kati ya kundi la makampuni ya Vigor Turkey Group ya Zanzibar na Global hospitals ya India.
“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua umuhimu wa sekta hizi kwa ustawi wa wananchi wa Zanzibar, ndio maana, tumeelekeza juhudi kubwa katika kuziimarisha kwa kuzifanyia mabadiliko, kutunga sera na sheria madhubuti na kuongeza bajeti ya mwaka kwa sekta hizi kila mwaka” Dk. Shein alisema.
Aliwaeleza viongozi na wageni waliohudhuria hafla hiyo kuwa amefurahishwa na uwekezaji huo wa aina yake katika sekta ya afya na kueleza matumaini yake kuwa hatua hiyo itazidi kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya nchini.
Dk. Shein alisisitiza kuwa azma ya serikali ni kuwa na miradi mingi mikubwa kama hiyo katika sekta zote na kwamba mswada mpya wa sheria uliopitishwa hivi karibuni kuhusu uanzishaji na uendeshaji ushirikiano baina ya Sekta ya Umma na Binafsi ni hatua muhimu katika kufikia azma hiyo.
Alitoa wito kuwepo ushirikiano wa karibu kati ya sekta binafsi na sekta ya umma katika afya na kutolea mfano kuwa hospitali hiyo ya TASAKHTAA kuwa na mashirikiano na hospitali kuu ya Mnazi mmoja.
“hospitali yenu itahitaji msaada mkubwa kutoka hospitali ya Mnazi Mmoja na kinyume chake hivyo mnahitaji kushirikiana”alieleza Dk. Shein na kuongeza kuwa hospitali hizo hazitakuwa washindani.
Katika hotuba yake hiyo alizidi kubainisha kuwa Serikali inaendelea kukamilisha mpango wake wa kuifanya hospitali ya Mnazi Mmoja kuwa ya rufaa ili iweze kutoa huduma nyingi zaidi na bora zaidi kwa wananchi.
Aliongeza kuwa kuimarika kwa huduma za afya nchini kutasaidia kupunguza idadi kubwa ya wagonjwa wanaopelekwa nchi za nje kupata matibabu mara kwa mara.
Dk. Shein ambaye kabla ya kuizindua hospitali hiyo alitembelea vitengo mbalimbali vya hospitali hiyo, alieleza kuvutiwa na vifaa na utalaamu uliopo lakini alisisitiza lugha na mahusiano mazuri kati ya watumishi wa hospitali na wagonjwa.
“Hospitali kama hii inatarajiwa kutoa huduma bora na nzuri, kufanya tafiti, na kuchunguza maradhi pamoja na kuwapa faraja wagonjwa kwa kuwahudumia kwa lugha nzuri” Dk. Shein alieleza.   
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman alisema Wizara imeupokea mradi huo kwa mikono miwili na kuutaka uongozi wa hospitali kuzingatia sheria na kanuni za uendeshaji wa hospitali zikiwemo za usajili wa watumishi wake katika bodi husika za kitalaamu pamoja na zile zinazohusu madawa.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini kwa niaba ya Waziri wa Fedha alisema sekta ya afya imo katika mpango kabambe wa serikali wa kutoa vivutio maalum vya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji zaidi.
Alibainisha kuwa hadi sasa sekta hiyo iko nyuma katika kuvutia wawekezaji tofauti na sekta nyingine kama ya utalii ambapo nchi inahitaji sana huduma katika sekta ya afya hivyo Serikali itaweka jitihada za makusudi  kuondoa hali hiyo.
“Inawezekana hatujaitangaza sana lakini pia yawezekana ni kutokana na ukosefu wa wataalamu na gharama kubwa za uwekezaji”alisema Dk. Mwinyi na kuongeza kuwa mradi wa TASAKHTAA umeonesha mfano katika uwekezaji katika sekta hiyo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kundi la makampuni ya Vigor Turkey Bwana Salim Turky aliwahakikishia viongozi na wageni waliohudhuria hafla hiyo kuwa uongozi wa hospitali hiyo umedhamiria kutoa huduma bora na na kwa gharama nafuu kwa wananchi wote.
“tutahakikisha wananchi wote wanapata huduma za matibabu na tayari baadhi ya wafanyabiashara wameahidi kusaidia gharama za wananchi ambao hawatakuwa na uwezo kabisa ili wasikose huduma”alibainisha Bwana Turky.
Alisema nia ya hospitali hiyo ni kushirikiana na watoa huduma wengine katika sekta hiyo zikiwemo hospitali za umma hivyo wakati wote.

Alizishukuru mamlaka mbalimbali za serikali kwa ushirikiano wao ambao hatimae hospitali hiyo imeweza kukamilika na kuzinduliwa tayari kuanza kutoka huduma kwa wananchi.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment