MissTanzania Doris Mollel Akitembelea Wodi ya Watoto Hospitali ya Muembeladu


Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo akiwa na Miss Tanzania Miss Doris Mellol (katikati) akitembela hospitali ya Muembeladu kuwatembelea Watoto Njiti mapacha watatu waliozaliwa katika hospitali hiyo.
Miss Tanzania Miss Doris Mollel akiwa na ujumbe wake wakitembelea hospitali ya wazazi ya Muembeladu Zanzibar kuwatembelea watoto waliozaliwa kabla ya kufika wakati wao jumla ya watoto watano wamezaliwa katika hospitali hiyo wote wakiwa mapacha.kwa mama wawili tafauti.
Miss Tanzania Doris Mollel akisalimiana na Muuguzi Mkunga Msaidi Bi Ruzuna Abdulrahim, na kulia Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo,  
Muuguzi Mgunga Msaidi Bi Ruzuna Abdulrahim akitowa maelezo kwa ujumbe wa Miss Tanzania alipofika hospitali ya muembeladu kutembelea Watoto Njiti, waliozaliwa katika hospitali hiyo hivi karibuni jumla ya watoto watano wamezaliwa wakiwa njiti.

Miss Tanzania Doris Mollel akiwaangalia Watoto walwili mapacha Njiti  Idrisa na Ismail waliozaliwa katika hospitali ya Wazazi Muembeladu na Mama Mwamvua Mohammad, Miss Tanzania pia na yeye ni Mtoto Njiti. amezaliwa akiwa hajatimiza miezi tisa na kuzaliwa miezi saba. katika hospitali ya Muhimbili

Miss Tanzania Diris Mollel akiwa na Watoto Njiti mapacha wawili Idrisa na Ismail wakati alipofika katika hospitali ya wazazi kutembelea Watoto Njiti

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi fedha shilingi laki moja  kwa ajili ya kumsaidia katika malezi ya watoto hao Idrisa na Ismail  Mama Mwamvua Mohammad aliyejifungua Watoto pacha wawili katika hospitali ya wazazi muembelea wakati hawajatimia miezi Tisa na kujifungua miezi Saba.
Miss Tanzania Doris Mollel akimsalimia Mama wa Watoto mapacha watatu (Njiti) Bi Kazija Batil Haji,akiwa na watoto wake Hassan, Hussein na Hafidh, aliyejivungua katika hospitali ya wazazi muembeladu Zanzibar wakati alipofika kuwaona watoto hao njiti akikumbuka na yeye alizawaliwa kabla ya miezi Tisa na kuzaliwa miezi Saba (Njiti) kushoto Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo na Mkunga Msaidizi wa hospitali ya Wazazi muembeladu Bi Ruzuna Abdulrahim.  , 
Miss Tanzania akiwachukua Watoto Njiti alipofika hospitalini hapo kuwatembelea Watoto Njiti Ikiwa ni moja ya kazi ya Angos yake kuwahudumia watoto Njiti.
Miss Tanzania Doris Mollel akiwa amewabeba Watoto mapacha  (Njiti) Hassan, Hussein na Hafidh, akiwa katika wadi ya wazazi hospitali ya muembeladu Zanzibar akiwa na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo   
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi fedha shilingi laki moja  kwa ajili ya kumsaidia katika malezi ya watoto hao Hassan, Husein na Hafidh, Mama Kazija Batil Haji,Mwamvua Mohammad aliyejifungua Watoto pacha wawili katika hospitali ya wazazi muembelea 
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment