Sherehe za Siku ya Wanawake Zafana Bwawani Hotel


Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa Zanzibalicious Women Group Bi Evelyne Wilson  Baruti, wakati alipowasili katika viwanja vya Salama Bwawani kuhudhuria sherehe za Siku ya Wanawake Duniani ilioadhimishwa na Kikundi hicho 
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Mama Mwanamwema Shein, akiangalia moja ya bidhaa za Wajasiriamali sabuni ya chokaa wakati wa sherehe hizo za Wanawake.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiangalia bidhaa za Wajasiriamali Wanawake wakati wa sherehe hiyo iliofanyika katika viwanja vya Salama Bwawani Zanzibar.
Mama Mwanamwema akitembelea mabanda ya maonesho ya Wanawake Wajasiriamali wakati wa sherehe hiyo ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa kila mwaka mwezi wa march.
Mama Mwanamwema Shein akipata maelezo kutoka kwa Mjasiriamali wa kikundi cha Organd Gold, wakati alipotembelea banda hilo.
Mwanamitindo Maarufu Tanzania Bi Asia Idaruos, akisalimiana na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, alipowasili katika viwanja vya Salama Bwawani Zanzibar.

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akipiga makofi wakati akiwasili katika ukumbi wa Mkutano huo kushoto Naibu Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe Thuwaiba Kisasi,Naibu Waziri wa Afya Mhe Mahmoud Thabit Kombo, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Abdallah Mwinyi Khamis,na kulia Mwenyekiti Mstaaf wa Kikundi Zanzibalicious Women Group Bi Ummikulthum Ansel na wa mwisho Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, wakiwa katika ukumbi wa Salama wakihudhuria sherehe hiyo.
   Wanawake wakiwa wakishangilia wakati wa Mke wa Rais wa Zanzibar kuingia katika ukumbi huo.
   Wanawake wakiwa wakishangilia wakati wa Mke wa Rais wa Zanzibar kuingia katika ukumbi huo.

Mwenyekiti wa Zanzibalicious Women Group Bi Evelyne Wilson Baruti, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kuchangia Kikundi hicho wakati wa kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani ilioandaliwa na kikundi hicho katika kuchangia mfuko wake.
Baadhi ya Wanawake waliohudhuria sherehe za Siku ya Wanawake Duniani na kuzindua mfuko wa Kikundi wakimsikiliza Mwenyekiti wa kikundi hicho.
Muweka Hazina wa Zanzibalicious Women Group Bi Sheikh Hilal akisoma risala ya Kikundi hicho wakati wa uzinduzi wa kuchangia Mfuko wa kikundi hicho wakati Sherehe za Siku ya Wanawake Duniani ilioadhimishwa na Wanawake wa Zanzibar.
Shuhuda wa matumizi ya dawa za kulevya Bi Arwa Hassan akitowa ushuhuda huo jinsi alivyoacha matumizi ya dawa za kulevya kwa kupata mafunzo katika nyumba za Sober House Zanzibar na kwa sasa ameacha matumizi hayo na kutowa Elimu kwa Wanawake wanaotumia dawa hizo akiwa ni Mama kiongozi wa Sober za Wanawake Zanzibar, Akiwataka Wanawake wanaotumia dawa waache mara moja na kujiunga na sober house.

         Baadhi ya Wanawake wakifuatilia hafla hiyo katika ukumbi wa salama bwawani Zanzibar.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo, akitowa mada kuhusiana na Mwanamke wakati wa sherehe za Siku ya Wanawake Duniani ilioadhimishwa kwa uzinduzi wa kuchangia Mfuko wa Zanzibalicious Women Group kwa chakula cha mchana. 
Wananchi walioshirikin katika sherehe za kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ilioadhimishwa katika ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.
Naibu Waziri wa Viwana Biashara na Masoko Mhe Thuwaiba Kisasi akizungumza katika hafla hiyo wa Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Salama Bwawani.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akihutubia na kuuzindua Mfuko wa Kikundi cha Zanzibalicious Women Group, wakati wa kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani ilioadhimishwa kwa Chakula cha hisani kuchangia mfuko huo, kulia Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko Zanzibar Mhe Thuwaiba Kisasi na kushoto Mwenyekiti Mstaaf Bi Ummukulthum Ansel,
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizindua Mfuko wa Zanzibalicious Women Group kwa kuchangia shilingi milioni tano, wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa salama bwawani Zanzibar kwa chakula chamchana cha hisani kuchangia mfuko huo  
        Naibu Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe Thuwaiba Kisasi akichangia mfuko huo.
Wanawake hawakuwa nyuma kuchangia Mfuko wao Bi Moza nae akichangia mfuko huo wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya uzinduzi wa mfuko huo. 
Miss Tanzania Mrembo Diris Mollel akichangia katika hafla hiyo ya sherehe za Siku ya Wanawake Duniani  
Warembo wakichangia mfuko huo baada ya kuguswa na maendeleo ya Wanawake Zanzibar katika kujikomboa na utegemezi.
           Kiongozi wa Kikundi cha Wasanii wa Maigizo Zanzibar nao wamechangia mfuko huo.
Mwanamitindo Mbunifu Tanzania Bi Asia Idarous akipiga Mnada moja ya Nguo alioidizaie kwa kutumia Kanga, Dira hilo limenunuliwa katika mnada huo na Mama Asha Balozi, kwa shilingi laki tano, na kumzawadia Bi Arwa Hassan, ambae ameacha matumizi ya dawa za kulevya Zanzibar na kwa sasa ni Kiongozi wa Sober House za Wanawake Zanzibar.

Picha kwa hisani ya Zanzinews
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment