Christian Bella Kuleta Mapinduzi ya Muziki wa Dance Inchini Tanzania

Mfalme wa Masauti Christian Bella ameachia Track yake mpya Nashindwa Audio pamoja na Video, Audio ya wimbo huo imefanywa chini ya Studio za Combination sound chini ya Producer man Walter na Video imefanyika Africa ya Kusini na director kutoka Bongo Adam Juma, Christian Bella amesema kuwa lengo la kwenda South Africa ilikua ni kufata location tu na pia amesema kuwa madirector wa Bongo wanauwezo mkubwa sana wa kufanya video nzuri kwa sasa isipokuwa hawana connection za TV kubwa za Africa na Nje ya Africa tofauti na Madirector wa SA ambao wana connection kubwa ya TV Kubwa hivyo wakikufanyia Video inafika Mbali zaidi.
Mbali na hilo Bella anatarajia kufanya show kubwa siku ya tarehe 18/4 na inategemewakufanyika pale escape one huku msanii Alice mwenye asili ya Kiganda lakini anaishi Sweden anatarajiwa kuwepo siku hiyo, Alice amefanya Track kama Mpita Njia na Juliana lakini pia amefanya Yabolingo Track ambayo imefanya vizuri sana hapa Tanzania na Est Africa kwa ujumla. Wasanii wengine watakao shiriki siku hiyo bado hawajajulikana lakini bella amesema kuwa anatarajia kufanya na wasanii wa THT na wengine ambao bado wako kwenye mazungumzo na haitokuwa band yeyote ya dance.
Share on Google Plus

About John Sambila

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment