HITMA YA MAREHEMU MZEE KARUME YASOMWA LEO ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai maara alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja kubhudhuria katika Hitma ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Iliyofanyika leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) akiwaongoza Viongozi mbali mbali pamoja na Wananchi katika Kisomo cha hitma ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika leo asubuhi.
Baadhi ya Viongozo wakisoma hitma akiwemo aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume(kushoto) Balozi Ali Karume katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika leo asubuhi.
Waislamu na wananchi mbali mbali wakiwa katika kisomo cha hitma ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika leo asubuhi.
Akinamama wa Mitaa mbali mbali ya Mji wa Unguja wakiwa katika kisomo cha Hitma ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja Iliyofanyika leo asubuhi.
Mke wa Rais Zanzibar Mama Mwanamwema Shein(katikati) akiwa na Mama Shadya Karume Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar(wa tatu kulia) Mama Fatma Karume (wa pili kulia) Mke wa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mama Zakia Bilali (kushoto) Bi Khadija Aboud (wa pili kushoto)Mjumbe wa Kamati Kuu wa CCM,katika hitma ya kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilali akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Hamid Ameir akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume, baada ya kisomo cha hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Balozi Ali Karume (Mtototo) kwa niaba ya familia akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma na dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Wake wa Viongozi wakiitikia dua iliyoombwa katika kaburi la Marehemu MzeeAbeid Amani Karume baada ya hitma iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja na kuhudhuriwa na waislamu mbali mbali Mjni na Vijijini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Viongizi wengine wakiitikia Dua iliyoombwa na Mufti Mkuu wa zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (kulia) baada ya kisomo cha hitma iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
Baba Askofu wa Anglikan wa Kanisa la Mkunazini Michael Hafidh akiomba dua wakati Viongozi mbali mbali waliofika katika kaburi la aliyekua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,baada ya kisomo cha hitma iliyosomwa leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.(Picha na Ikulu, Zanzibar.)
 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein leo ameongoza hitma ya kumuombea dua Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu mzee Abeid Amani Karume, iliyofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini Zanzibar.
 
Hitma hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Kharib Bilal, Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Sita, Mhe. Amani Abeid Karume, Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.
 
Viongozi wengine walihudhuria katika hitma hiyo ni  Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabhi, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Sheikh wa Mkoa wa Dar-es- Salam Sheikh Mussa Salum na viongozi wengineo.
 
Wengine ni viongozi wa serikali zote mbili na viongozi wastaafu, viongozi wa vyama vya siasa, Masheikh kutoka Zanzibar na Tanzania Bara, Wabunge na Wawakilishi, wananchi kutoka sehemu mbali mbali pamoja na Mabalozi wadogo waliopo hapa Zanzibar.
 
Hitma hiyo ya kumuombea dua Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pia ni miongoni mwa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa ilitanguliwa na Qur-an tukufu, iliyosomwa na Ustadh Sharif Muhidin na kuongozwa na Sheikh Jafar kutoka Masjid Noor Mohammad,iliopo Kwa Mchina Mwanzo.
 
Mara baada ya hitma hiyo, Sheikh Mkoa wa Dar-es-Salaam, Sheikh Mussa Salum alitoa mawaidha na kumuelezea marehemu mzee Abeid Amani Karume kuwa ni kiongozi aliyepigania maendeleo ya wananchi wa Zanzibar na kumuombea MwenyeziMungu ampe makaazi mema Peponi.
 
Akieleza kuhuhu umuhimu wa siku hii, Sheikh Mussa alisema kuwa siku ya leo ni muhimu sana kwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwa lengo la kumuombea dua Marehemu Karume pamoja na mashujaa wengine.
 
Aidha, Sheikh Mussa alitumia fursa hiyo kukumbusha juu ya umauti na kusisitiza kuwa ni  jambo ambalo litafika kwa kila kiumbe alichokiumba MwenyeziMungu na kusisitiza kuwa ni vizuri mwanaadamu akakumbuka asili yake na hatma yake.
 
“Kifo ni onyo, kifo ni mawaidha na kifo ni mazingatio...kutokana na hali hiyo kuna kila sababu ya kutenda mema, kuwa na mahaba, kuwa na udugu wa kiimani.. huku tukiendelea kumuombea dua mzee wetu huyu kwani yeye ameonja umauti kama ilivyoeleza Qur-an ikiwa na maana kuwa roho yake bado iko hai” alisema Sheikh Mussa.
 
Pamoja na hayo, Sheikh Mussa katika kutilia mkazo suala zima la udugu wa kiimani alitoa pongezi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuendelea kusimamia Serikali ya Mapindui ya Zanzibar yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa ambayo imewafanya Wazanzibari kuimarisha udugu wao na kuwa kitu kimoja kama Uislamu unavyotaka.
 
Alisema kuwa hatua hiyo imezidisha umoja sambamba na kuimarisha amani na utulivu uliopo na kuifanya Zanzibar kuwa tulivu na kusisitiza kuwa huo ndio udugu wa kiimani.
 
Baada ya kisomo hicho cha hitma ambacho hufanyika kila mwaka inapofika tarehe 7, Aprili, viongozi hao na wananchi waliohudhuria katika hitma hiyo walimuombea dua, marehemu mzee Abeid Karume katika kaburi lake lililopo pembezoni mwa afisi hiyo ya CCM Kisiwandui dua iliyoongozwa na viongozi wa dini tofauti akiwemo Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Kabhi, Askofu Michael Hafidh kutoka Kanisa la Anglikana Zanzibar na Bhaguan Suria (Mshamba) aliyesoma kwa niaba ya Wahindu.
 
Viongozi na wanafamilia waliweka mashada ya maua katika kaburi la marehemu mzee Abeid Amani Karume akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohammed Kharib Bilal, Mzee Hamid Ameir aliyeweka shada la maua akiwakilisha wazee walioshiriki Mapinduzi ya Januari 12, 1964.
 
Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Luteni Jeneral S.A. Ndomba, Balozi Ali Karume aliyewakilisha familia ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume na Balozi mdogo wa China anayefanya kazi zake hapa Zanzibar Mhe. Xie Yualing aliyewawakilisha Mabalozi wenzake wa hapa nchini.
 
Aidha, Mama Mwanamwema Shein aliungana na akina mama wengine katika hitma hiyo katika Afisi hiyo ya CCM Kisiwandui, akiwemo mjane wa marehemu mzee Abeid Karume, Mama Fatma Karume, Mama Asha Bilali,Mama Zakia Bilal, Mama Asha Balozi na Mama Pili Balozi, Mama Shadya Karume na viongozi wengine wanawake wa kitaifa wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Wawakilishini na wananchi kutoka sehemu mbali mbali ya Zanzibar na Tanzania Bara.
 
April 7, 1972 ndiyo siku aliyouawa Rais wa Kwanza wa Zanzibar marehemu Mzee Abeid Amani Karume na wapinga maendeleo nchini ambapo hivi leo imetimia miaka 43 tokea utokee msiba huo.
 
(Picha / Habari: Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar)
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment