MABASI YAPATA AJALI TANGA NA MOROGORO NA KUUWA WATU KADHAA

Basi la Ngorika lenye namba za Usajili T770 BKW lililokuwa kitoka jijini Dar es Salaam kwenda Arusha na lile la Kampuni ya RATCO T 274 DCP Tanga kwenda Dar es Salaam yamegongana uso kwa huso na kulihusisha gari lingine dogo aina ya Toyota Pass T 628 CXE na kusababisha vifo vya abiria 10 na majeruhi. Ajali hiyo ilitokea eneo la Mbweni Mkata, wilayani Handeni mkoni Tanga. 

Inaelezwa kuwa basi la Ratco lilgongana kwanza na gari dogo na kisha kwenda kugongana uso kwa uso na basi la Ngorika ambapo abiria 8 walifariki katika basi hilo na wawili waliokufa walikuwa katika gari dogo wakipeleka mgonjwa hospitali.

Wakati huo huo habari kutoka Morogoro zinaarifu kuwa Basi mali ya kampuni ya Happy Nation lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kwenda Mbeya limepata ajali eneo la Kikwaraza Mikumi na kuuwa watu wawili na kusababisha majeraha kwa abiria wengine 48.
Basi la Ngorika likiwa limeharibika vibaya.
Gari dogo aina ya Noah lililohusika katika ajali ya Tanga na abiria wake wote waliokuwa wa fami;lia moja kuripotiwa kufa. Habari kwa hisani ya Father Kidevu
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment