MEYA WA MANISPAA YA KINONDONI ASHINDA TUZO YA MEYA BORA TANZANIA

Rais Jakaya Kikwete akikabidhi tuzo ya Meya Bora Tanzania kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda baada ya kushinda tuzo hiyo kitaifa iliyoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini (ALAT) katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Kulia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Agrey Mwanri.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza baada ya kukabidhi Tuzo ya Meya Bora Tanzania, Yusuph Mwenda (kulia) baada ya kushinda tuzo hizo zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini (ALAT) katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Tom Boghols na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia (wa pili kushoto). 
Rais Jakaya Kikwete akitoa maelekezo kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kulia) kuhusu namna bora ya matumizi ya trekta baada ya kumkabidhi Meya huyo baada ya kushinda Tuzo ya Meya Bora Tanzania kwenye hafla iliyofanyika Dar es Salaam hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki na Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Tom Boghols (wa pili kulia).
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akijaribu kuendesha trekta alilokabidhiwa na Rais Jakaya Kikwete baada ya kushinda tuzo ya Meya Bora Tanzania. 

Na Mwandishi Maalum,
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda ameshinda Tuzo ya Meya Bora Tanzania na kuzishinda Halmashauri 168 zote nchini.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda amesema siti ya kushinda tuzo hiyo ni kufanya kazi kwa pamoja kati yake Madiwani, Watendaji na kuwahsirikisha wananchi wake.

Meya Mwenda alisema kuwa Halmashauri yake imekuwa ikifanya kazi kwa uwazi zaidi kwa kuwashirikisha wananchi wake katika mikakati ya kimaendeleo ikiwemo kuwashirikisha katika miadi mbalimbali ya Halmashauri hiyo na hivyo kujikuta kazi yake inakuwa rahisi na kupata mafanikio makubwa kwa muda mfupi.

Mwenda alisema kuwa Manispa yake imekuwa mstari wa mbele katika kusimamia na kuitekeleza miradi yake kwa bidii kubwa ikiwemo ukusanyaji mapato na usimamizi mzuri wa matumizi ya mapato hayo katika miradi hiyo.

“Ushirikiano ‘team work’ kati yangu na madiwani, Madiwani na Watendaji, Ofisi ya Mkuu wa Wialaya na Mkuu wa Mkoandio siri ya mafanikio. Lakini kubwa zaidi ni wananchi wenyewe, kupitia wao tumeweza kuwa na mendeleo zaidi.” Alisema Mwenda.

Aidha Meya Mwenda alisema kuwa Halmashauri yake imefanikiwa kufikia malengo yake kutoka na kuongezeka kwa mapato ya ndani kwa aslimia 360 kutoka shilingi Bilioni 10 mwaka 2011/ 2011 mpaka kufikia Bilioni 36 mwaka jana na kuiwezesha Manispaa hiyo kusimamia vema miradi yake yenyewe.

Aliitaja miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa Barabara, Madara, Zahanati, Shule, matumizi ya Teknohama pamoja na ujenzi wa Kituo kikubwa cha daladala cha kisasa cha Sinza ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 4.06.

Aidha alisema Halmashauri yake imeweza kuongeza fedha za miradi yake ya maendeleo kutoka Bilioni 3.2 kwa mwaka 2011 mpaka kufikia Bilioni 16 na hivyo kuifanya kuwa ya kwanza nchini kusimamia miradi yake kwa fedha za mapato ya ndani kwa asilimia kubwa.


Hii ni mara ya kwanza kufanyika kwa shindano la Tuzo za Meya Bora Tanzania chini ya Jumuiya ya Serikali za Mitaa nchini (ALAT) ambazo zilikuwa katika makundi mawili makuu ambayo ni Tuzo ya Maendeleo ya Halmashauri na Tuzo ya Jumla ambazo zilifanyika juzi na kuhudhuriwa na Rais Jakaya Kikwete. 

Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment