WACHEZAJI VETERANI WA FC BARCELONA WAMTEMBELEA RAIS KIKWETE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wachezaji maveterani wa timu ya Barcelona wakati walimpomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam .
 Mchezaji nyota wa zamani wa Holland  na kocha wa Timu ya veterani ya Barcelona Johann Cruyft akimkabidhi jezi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam jana
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji maveterani wa timu ya Barcelona walipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam jana. Picha na Fred Maro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumamosi, Aprili 11, 2015, amekutana na wachezaji nyota wa klabu ya soka la Barcelona ya Hispania katika shughuli iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam. 
Wachezaji hao wakiongozwa na nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1974 nchini Ujerumani Johann Cruyff pamoja na nyota mwingine wa klabu hiyo na nchi hiyo, Patrick Kluivert wamekaa Ikulu kiasi cha dakika 40 kabla ya kuondoka kwenda Uwanja wa Taifa kwa mchezo wao na nyota wa zamani wa Tanzania. 
Mheshimiwa Rais Kikwete amewashukuru wachezaji hao kwa kukubali kutembelea Tanzania na kusema kuwa wanakaribishwa tena kuja nchini kwa muda mrefu zaidi.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment