MGOMO WA MADEREVA WA MABASI NA DALADALA ULIODUMU KWA SIKU MBILI HATIMAYE WAMALIZIKA

 
Mh mbowe alipata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa madereva hao.Mh Mbowe alipotaka kuzungumza na madereva hao microfone zote zilizimwa na kufichwa kusikojulikana jambo ambalo lilifanya ashindwe kusikika kwa madereva hao na kuamua kumtoa nje na kusukuma gari yake hadi maeneo ya shekilango na kurudi ofisini.

Hatimaye mgomo wa madereva uliodumu kwa siku mbili umemalizika leo kwa masharti baada ya majadiliano kati ya mkuu wa wilaya ya Kinondoni na maderevaNa Bakari Issa Majeshi
Mgomo wa Madereva uliodumu  kwa takriban siku moja na ushee, hatimaye umepata muafaka baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda (pichani) kufanikiwa kuusuluhisha kwa kusaini makubaliano na Uongozi wa Chama cha Madereva.
Makubaliano hayo yaliitaka Serikali kuboresha  Mikataba kwa Madereva, malipo kwa madereva hao, pamoja na tatizo la ukaguzi wa magari ili kuondoa usumbufu kwa madereva hao, na kuiomba Serikali kufanya ukaguzi huo kwa siku moja tu.
Akizungumza na Madereva hao, Mhe, Makonda amewataka Madereva hao kuachana na mgomo huo  na kuwaahidi Madereva hao kuyafanyika kazi madai yao katika muda ambao wamekubaliana usiozidi saa 4 asubuhi kesho.

Aidha, Mhe Makonda amesema katika madai hayo imeundwa Tume ambayo itashughulikia madai hayo pamoja na kuwahakikishia Madereva hao kuwepo na mwakilishi katika Tume hiyo iliyoundwa, ambayo itajadili masuala ya Mkataba, malipo, matibabu pamoja na suala la kusoma kwa Madereva hao.
Pia Makonda amelitaka Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni kuwaachia Madereva ambao tayari walikua wamekamatwa kutokana na kuonekana kufanya fujo katika mgomo huo katika Soko la Urafiki jijini Dar es Salaam. 
Kwa Upande wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Madereva, Bw. Rashidi Salehe amemuomba Mkuu wa Wilaya kutatua madai ya Madereva hao ili kuondoa mgomo ambao unakwamisha usafirishaji wa abiria.
Share on Google Plus

About JG Blog Team

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment