YANGA YAKABIDHIWA KOMBE LA UBINGWA WA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA 2014 - 2015Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2014- 2015, Yanga wakishangilia ubingwa wao huo mara baada ya kumalizika kwa mtanange wao dhidi ya Azam FC, uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo.Mtanange huo ulimalizika kwa Azam kushinda Bao 2-1.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, MMG.
Mgeni Rasmi katika Mchezo huo, Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Mh. Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi Nahodha wa Timu ya Yanga, Nadir Haroub cheti cha pongezi kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani, Sepp Blatter kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara 2014 - 2015.Kushoto ni Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji.
Mgeni Rasmi katika Mchezo huo, Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Mh. Dkt. Fenella Mukangara akimpongeza Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa baada ya kuchaguliwa kuwa Mchezaji bora wa mwezi wa nne.
Wachezaji wa Timu ya Yanga wakiingia uwanjani tayari kwa kukipiga na timu ya Azam FC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
Mwali kabla ya kukabidhiwa kwa wenyewe.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment