Kilimanjaro V Yawasili Zanzibar na Kuaza Safari Zake Mwishoni mwa Wiki Hii.

Kampuni ya Boti za Azam Marine Zanzibar yatowa Boti Mpya ya Kilimanjaro V,iliowasili juzi katika bandari ya Zanzibar na inategemewa kuaza kutoa huduma ya Usafiri kati ya Zanzibar na Dar-es-Salaam mwishoni mwa wiki hii baada ya kukamilisha taratibu zote za kisheria na kuaza kutowa huduma hiyo. Ikiwa katika bandari ya Zanzibar leo.Ina uwezo wa kuchukua Abiria 550, inachukua masaa maskamu lisaa moja na nusu mpaka Dar. 
 Kepteni wa Boti Mpya ya Kilimanjaro V Thomas Buhatwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya Zanzibar kuhusiana na huduma zinazopatikana katika boti hiyo mpya na kutowa maelezo ya vyombo vya kisasa viliomo katika boti hiwa wakati wa kuitembelea boti hiyo ikiwa katika bandari ya Zanzibar leo mchana.
Kapteni Thomas Buhatwa akionesha mitambo ya kisasa ya boti hiyo inayoonesha hali halisi ya bahari wakati wa safari zake akiwa katika chumba cha makepteni katika biti hiyo wakati waandishi walipotembelea biti hiyo mpya. 
Meneja Mkuu wa Azam Marine Ndg Hussein M Said, akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibarv wakati waandishi hao walipoitembelea Boti hiyo Mpya na kupata maelezo kutoka kwa Meneja, Boti hiyo ikiwa katika bandari ya Zanzibar na kuelezea uina uwezo wa kuchukua abiria 550 kwa wakati mmoja na mizigo pia amesema ina uwezo wa kusafiri kati ya Zanzibar na Dar kwa muda wa saa moja na nusu, Amesema inatarajiwa kutowa huduma mwishoni mwa wiki hii ikikamilisha taratibu zote zilizobaki katika vyombo husika.
Sehemu ya VIP One ikiwa na Video katika viti vyake vyenye uwezo wa kulala wakati abiria wakiwa safarini. 
                                                   Sehemu ya VIP kama inavyoonekana
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Marine Ndg Hussein M Said, akizungumza na Mwakilishi wa kampuni ya RDM- Marine Engineer ya Australia Egn Kerry Williams, wakiwa katika boti hiyo baada ya ukaguzi na majaribio ya Boti hiyo yaliofanyika hadi katika visiwa vya Chumbe na kurudi baada ya ukaguzi uliofanywa na ZAM.


Share on Google Plus

About JG Blog Team

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment