KINANA AMALIZA ZIARA YA SIKU 10 MKOANI KAGERA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Buharamulo mara baada ya kuwasili kwenye kata ya Nyabugombe ,wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya wilaya ya Biharamulo.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wazee wa kata ya Nyakahura,wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akielekea kwenda kuona mradi wa maji uliopo Nyakahura ambao ulitegemewa kusaidia vijiji vinne ,shule, vituo vya afya na polisi, badala yake unatoa huduma kwenye shule moja tu,mradi uliogharimu shilingi za Kitanzania bilioni 1.4
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kagera, Mhe John Mongella mara baada ya kukagua mradi wa maji uliopo Nyakahura uliogharimu pesa za Kitanzania shilingi bilioni 1.4.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma bango lenye malalamiko ya kukosa maji lilioandikwa na wakazi wa kata ya Nyakahura kwenye mkutano wa hadhara .

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wakazi wa Nyakahura.
 Katibu Mkuu wa CCM akitafakari mambo kwenye mkutano wa hadhara Nyakahura
 Ndugu Majaliwa Issa akiuliza swali kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Nyakahura Mizani, wilaya ya Biharamulo ambapo alitaka kujua hatua gani zinachukuliwa kwa waliochakachua mradi mkubwa wa maji.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nyakahura ambapo aliwaambia wananchi hao waache kuchagua viongozi kwa ushabiki,Katibu Mkuu aliwaeleza wananchi hao kuwa Mbunge wao alipaswa kuwa wa kwanza kufuatilia mradi huo pamoja na madiwani lakini hawakufuatilia kitu mpaka mradi umepoteza fedha nyingi na wananchi kukosa maji.
 Katibu Mkuu wa CCM akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa wa kijiji cha Busil,wilaya ya Biharamulo.
 Katibu Mkuu akisalimiana na wananchi wa Busil. Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Busil.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi wa Busil.
 Mwenyekiti wa kijiji Ndugu Enock Kulindwa.

 Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe.John Mongella akizungumza na wanakijiji cha Kikoma wilaya ya Biharamulo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kikoma ambao waliusimamisha msafara wake wakitaka majibu ya hoja zao.
 Meneja wa Tanesco wilaya ya Biharamulo Ndugu Ernest Miliyango akielezea namna wanavyoendesha shughuli za kuzalisha umeme mara baada ya kupokea mashine mpya ya uzalishaji umeme kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) na Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea taarifa ya ujenzi wa Wodi ya Wazazi katika kituo cha afya cha Rukaragata kutoka kwa Dk. Donasian Kamara.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Dk. Donasian Kamara mara baada ya kumaliza kukagua Wodi ya Wazazi Rukaragata, Biharamulo mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM akipokea taarifa ya ujenzi wa shule ya ARahman kutoka kwa Katibu wa Shule hiyo Sheikh Masoud Sadala.
 Katibu Mkuu wa CCM akishiriki kuweka dirisha katika moja ya madarasa ya shule ya ARahman ,Biharamulo mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule ya kiislam ya ARahman ,Biharamulo mjini.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi waliojitokesa kwenye mkutano wa hadhara Soko jipya Biharamulo.


 Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mhe.Darry Ibrahim Rwegasira akiwasalimu wananchi wa Biharamulo mjini waliojitokeza kwa wingi kuja kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera Ndugu Yahaya Kateme akiwasalimia wakazi wa Biharamulo mjini.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake mkoa wa Kagera Revina Jovin akiwasalimia wakazi wa Biharamulo mjini.
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Biharamulo akiwasalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Biharamulo mjini na kuwaambia CCM pekee ndio ina sera zinazotekelezeka na zenye kuleta maendeleo kwa wananchi.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha zawadi aliyopewa na CCM mkoa wa Kagera mara baada ya kumaliza ziara ya siku 10 mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Biharamulo mjini ikiwa siku ya mwisho ya ziara ya siku 10 mkoani Kagera ambapo alizungumzia changamoto mbali mbali zikiwemo za Bei ya Kahawa, Leseni za Bisahara na Boda Boda, Urahisishwaji wa Biashara mipakani , Katibu Mkuu aliwataka wananchi wa Biharamulo kuacha siasa za kishabiki badala yake kuchagua viongozi wanaofaa na watakaoleta maendeleo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati akihutubia wakazi wa Biharamulo mjini.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment