BOBBI KRISTINA BROWN AFARIKI DUNIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 22

Bobbi Kristina Brown, mtoto wa wanamuziki wawili maarufu na waliowahi kutamba sana enzi zao, marehemu Whitney Houston na Bobby Brown, amefariki dunia leo tarehe 26 Julai 2015 huko Duluth, Georgia nchini Marekani akiwa amezungukwa na wanafamilia. Bobbi Kristina amefariki akiwa na umri wa miaka 22. Hiyo ni kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii
Mauti yamemfika Bobbi Kristina takribani miezi 6 tangu alipokutwa bafuni akiwa hajitambui tarehe 31 January mwaka huu. 

Bobbi Kristina alizaliwa tarehe 4 Machi mwaka 1993 huko Livingston, New Jersey. Pumzika kwa amani.

Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment