EDWARD LOWASSA AJIUNGA RASMI CHADEMA NA AKABIDHIWA KADI

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya uanachama wa chama hicho,Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa leo katika hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.Picha na Ahmad Michuzi wa Michuzi Media
 Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akizungumza na mamia wakati wa kutangaza adhima yake ya kujiunga na Chadema katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya kujunga kwake katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
 Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa (mwenye umvi) akiwa na viongozi wa UKAWA katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimpa kadi ya uanachama Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Regina Lowassa leo katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
 Mh.Lowassa akiingia kwenye Hoteli Bahari Beach  kwa ajili ya kutangaza adhima yake ya kujiunga na UKAWA. Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa ametangaza kujiunga rasmi na Umoja wa Katiba (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) .
 Mh.Edward Lowassa akiwa katika hadhara ya mamia kujibu maswali katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
 Mh.Lowassa akiwa na viongozi wa UKAWA  katika Hoteli ya Bahari Beach Hoteli jijini Dar es Salaam jioni ya leo mara baada ya kutangaza rasmi azma yake ya kujiunga na ukawa.
 Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa katika Hoteli ya Bahari Beach Jijini Dar es Salaam jioni hii alipokuwa akitangaza azma yake ya kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA.
Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba  katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Share on Google Plus

About JG Blog Team

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment