KATIBU MKUU KIONGOZI MHE. OMBENI SEFUE ATEMBELEA OFISI ZA UBALOZI WA TANZANIA, UINGEREZA


Katibu Mkuu Kiongozi, Mheshimiwa Balozi Ombeni Sefue, akiweka saini kwenye Kitabu cha Wageni Ofisini kwa Balozi wa Tanzania, Uingereza.

Katibu Mkuu Kiongozi, Mheshimiwa Ombeni Sefue, akizungumza na Maafisa wa Ubalozi, alipotembelea Ubalozini hapo. Mheshimiwa Katibu Kiongozi alikuwa nchini Uingereza katika Ziara yake ya kikazi ambayo iliandaliwa na Taasisi ya ESAMI kuhudhuria semina ambayo ilikuwa na lengo la kuwakutanisha Viongozi wa Vyama vya Siasa na Watendaji wa Serikali, kuangalia changamoto mbalimbali ambazo wanakumbana nazo na muingilio wake katika utendaji wa kazi zao za kila siku.

Mheshimiwa Katibu Mkuu Kiongozi akiwa pamoja na Balozi wa Tanzania, Uingereza, Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe, kwenye Ofisi za Ubalozi Tanzania London, Uingereza.

Katibu Mkuu Kiongozi, Mheshimiwa Balozi Ombeni Sefue (waliokaa-kushoto) na Balozi wa Tanzania Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe (waliokaa-kulia), wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi. Mheshimiwa Katibu Mkuu Kiongozi alitembelea ofisi hizo za Ubalozi na kupata nafasi ya kuzungumza na Maafisa hao mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi nchini Uingereza
Mr. Rashid Dilunga
ICT Manager

Tanzania Trade Centre
Tanzania High Commission
3 Stratford Place
London W1C 1AS
Tel: 0207 7588070
Fax: 0207 7588073
Email: dilunga@tanzatrade.co.uk
Web: www.tanzatrade.co.uk
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment