Mhe Hamad Rashid Zanzibar achukua Fomu ya Kugombea Urais kwa tiketi ya Chama cha ADC.

Aliyekuwa Wanachamna wa CUF na Mbunge wa jimbo la Wawi kisiwani Pemba, ambaye kwa sasa amehamia chama cha ADC, Hamad Rashid Mohamed leo amechukuwa fomu ya kugombe urais wa Zanzibar kupitia chama cha ADC, kulia ni kamishna wa ADC kanda ya Pemba Saidi Seif akimkabidhi mgombe huyo Fomu
MGOMBEA urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ADC, Hamad Rashid Mohamed katitaki akizungumza na wananchi na wanachama wa ADC mara baada ya kuchukuwa fomu ya Urasi huko katika ofisi za chama hicho Wawi kibegi kisiwani Pemba.

Na Abdi Suleiman na Abdi Shamnah,PEMBA.
ALIYEKUWA mwanachama wa chama cha CUF na mbunge wa jimbo la wawi kisiwani Pemba, ambaye kwa sasa amehamia chama cha ADC Hamad Rashid Mohamed, Leo amechukuwa fomu ya kugombea urais wa Zanzibar kupitia chake hicho.

Fomu hiyo aliyokabidhiwa leo na kamishna wa ADC Kanda ya Pemba, Said Seif huko katika ofisi za chama hicho Wawi kibegi Wilaya ya Chake Chake Pemba.

Akitoa nasaha zake Mara baada ya kuchukuwa fomu hiyo, Mgombea huyo Hamad Rashid, alisema hatua hiyo ya kuchukuwa kweke fomu inalenga kuleta mabadiliko makubwa ya kisiasa Zanzibar.

Alisema kuwepo kwa chama hicho ni kuondosha dhana iliyojengeka miongoni mwa wananchi wa Zanzibar, pamoja na viongozi wa vyama vya upinzani kwamba vyama vya CCM na CUF ndio vyama vyenye uhalali wa kuongoza nchi.

Alisema hatua ya wananchi wa Pemba kujitokeza na kumpokea kwa wingi ni thibitisho tosha kwa wananchi kuwa wamejenga imani nayeye na wamekubali mabadiliko ili kuelekeza nchi hiyo katika maendeleo ya kweli.

"Leo ni siku ya historia katika chama cha ADC tokea miaka tatu kuwepo kwao, kimeweza kutoa mabadiliko makubwa kufikia kupatikana mgombe wa urais wa Zanzibar" alisema Hamad Rashid.


Aidha aliwapongeza wananchi na viongozi wa ADC kwa ujasiri wao mkubwa wa kuanzisha chama hicho, huku baadhi ya watu na viongozi wa upinzani wakiona hatua hiyo kwamba ni dhambi.
Aliwataka wananchi kisiwani Pemba kuendeleza imani na chama hicho na kuondokana na dhana kwamba CUF ndio chama pekee chenye uwezo wa kuwapelekea maendeleo, huku akibeza kisiwa hicho kubaki nyuma kimaendeleo.

Mgombea huyo wa ADC anatarajiwa kurudisha fomu hiyo Julai 28 mwaka huu, Kwa katibu mkuu wa chama hicho Unguja, kabla ya kuchukuwa fomu ya Serikali ya kugombea urais wa Zanzibar.

Mapema kamishna wa ADC kanda ya Pemba Said Seif alimshukuru mgombea huyo kwa ujasiri na uamuzi wake wa kujitokeza kuchukuwa fomu ya kugombea urais wa Zanzibar kupitia ADC.

"Hiki ni kitendo cha kihistoria kwa mlezi wetu kujitokeza kuchukuwa fomu, sisi wananchi na wanachama wa ADC tuko pamoja na yeye"alisema.

Alisema mgombea huyo ni kiongozi shupavu na aliyekomaa kisiasa, huku wananchi wakiwa na matumaini makubwa kutoka kwake katika kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye nafasi ya urais wa Zanzibar.
Share on Google Plus

About JG Blog Team

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment