Taswira katika mkutano wa CCM jana kumchagua mgombea Urais

Waasisi wa mbali mbali wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi ambao umefanya uchaguzi wa kumchagua Mgombea Urais kwa nafasi ya CCM uliofanyka jana katika ukumbi mpya Makulu nje ya Mji wa Dodoma,[Picha na Ikulu.
 Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM Magufuli akisalimiana na wanachama mara alipoingia katika ukumbi wa Mkutano kabla ya Uchaguzi utakaoweza kutoa ushindi kati ya Wagombea watatu ambapo wengine ni Bi Anima Salum Ali na Bi Asha Rose Migiro,uchaguzi huo umefanyika jana katika  ukumbi mpya wa CCM Makulu Nje ya Mji wa Dodoma, [Picha na Ikulu.]
 Wanachama wa CCM wa Mikoa mbali mbali wakisherehekea kwa fuaraha wakati wa Mkutaano maalum wa CCM 2015 uliofanyika katika ukumbi mpya Makulu Nje ya Mji wa Dodoma jana,chini ya Mwentyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, [Picha na Ikulu.]

 Baadhi ya wajumbe wa  Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi mwaka 2015  wakifuatilia kwa makini harakati za uchaguzi wa Mgombea Urais kwa nafasi ya CCM ambapo wagombea watatu watapigiwa kura kumpata mgombe mmoja atakae wakilisha CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao,mkutano huo umefanyika jana katika ukumbi mpya wa CCM Makulu Nje ya Mji wa Dodoma, [Picha na Ikulu.]
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM ZanzibarVuai Ali Vuai mara alipowasili katika  Mkutano Mkuu Maalum wa CCM 2015 katika ukumbi mpya wa Makulu Nje ya Mji wa Dodoma jana,[Picha na Ikulu.]


 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wanachama alipoingia katika ukumbi mpya wa Makulu Nje ya Mji wa Dodoma katika Mkutano Mkuu Maalum wa 2015,[Picha na Ikulu.]

 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Viongozi wengine wakiimba wimbo wa CCM wakati wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM 2015 uliofanyika jana katika ukumbi mpya wa Makulu Nje ya Mji wa Dodoma,[Picha na Ikulu.]

 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiongoza mkutano Mkuu Maalum wa CCM 2015 katika ukumbi mpya wa Makulu Nje ya Mji wa Dodoma uliofanyika jana,wengine kutoka kushoto Makamo wa Rais wa jamhuri ya Muungao Dkt.Mohamed Gharib Bilali,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) Makamo Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula na katibu Mkuu CCM Taifa Abdulrahman Kinana,
 [Picha na Ikulu.]

Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment