VIKAO VYA CCM VINAVYOENDELEA DODOMA

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(wa pili kushoto) akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM ambacho kinateuwa majina 5 ya wagombe Urais wa Tanzania kupitia CCM katika  Ukumbi wa mikutano wa Makamo Makuu ya CCM Dodoma leo,(kushoto) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Makamo Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa wa CCM Zanzibar akifuatana na wasaidizi wake alipokuwa akiingia katika Ukumbi wa Mkutano Maalum wa kamati Kuu ya CCM Taifa uliofanyika leo Mjini Dodoma
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana akitoa taarifa katika Mkutano Maalum wa Kamati Kuu ya CCM Taifa mbele ya Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(wa pili kushoto) ambao utateuwa majina matano ya wagombea urais wa Tanzania kupitia CCM,wengine Makamo wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Makamo Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula (kulia)katika  Ukumbi wa mikutano makamo Makuu ya CCM Dodoma leo
Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa NEC wakibadilishana mawazo wakati wakisubiri uteuzi wa majina matano kutoka Kikao Maalum cha Kamati Kuu kinachoteuwa majina hayo leo ambapo kesho yatapigiwa kura kuchagua jina moja la Mgombe Urais kupitia CCM 
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pansdu Ameir Kificho akisalimiana na Mzee Cleopa Msuya nje ya Ukumbi wa Mikutano kabla ya kuanza kikao cha Mkutano Maalum wa kamati Kuu ya CCM Taifa wenyeuwezo wa kuteuwa majina matano ya wagombe Urais kupitia CCM hatimae majina hayo kupigiwa kura kumpata mgombea Mmoja katika Mkutano Mkuu Maalum wa Halamashauri Kuu ya Taifa Nec
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment