DK MAGUFULI AZIDI KUWACHANGANYA WAPINZANI KAMPENI ZA URAIS NJOMBE

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akihutubia katika mkutano wa hadhara wa kampeni kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, Philip Mangula akihutubia kwa kumnadi Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli  katika mkutano wa hadhara wa kampeni kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akimtambulisha Naibu Waziri wa Ujenzi, ambaye anagombea ubunge Jimbo la Njombe Kaskazini, Gerson Lwenge katika mkutano wa hadhara wa kampeni wilayani Wanging'ombe, mkoani Njombe
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya  Shilole akitumbuiza leo kwenye mkutano wa kumnadi Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
Dk Magufuli akitoa shukrani kwa viongozi wa CCM Mkoa wa Mbeya baada ya kumaliza ziara mkoani humo  na kuanza kampeni katika Mkoa wa Njombe
  Dk.Magufuli akijinadi kwa wananchi na kutoa ahadi  katika nKijiji cha Igoma, Mbeya Vijijini aliposimama kwa muda akielekea Makete mkoani Njombe kuendelea na kampeni.  Akichaguliwa ameahidi kujenga barabara  ya lami ya Njombe hadi Mbeya kuptia Makete na kijijini hapo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Wananchi wakishangilia baada ya kuelezwa na Dk Magufuli kuhusu ijenzi wa barabara ya lami itakayopita kijijini hapo
 Wananchi wakimshangilia Dk Magufuli kijijini hapo
 Dk Magufuli akijinadi katika Kijiji cha Ilungu Mbeya Vijijini mpakani na Mkoa wa Njombe
 Wananchi wakishangilia huku wakiwa na vipeperushi vyenye picha za Dk Magufuli
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), ambaye pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Makete,  Binilith Mahenge akimpigia debe Dk Magufuli pamoja na Mgombea ubunge wa Jimbo la Makete, Norman Sigalla.
 Dk. Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano uliofanyika Iwawa wilayani Makete
 Dk Magufuli akimtambulisha mgombea ubunge jimbo la Makete, Dk Norman Sigalla katika mkutano wa kampeni uliofanyika Iwawa Makete
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wenye Ulemavu nchini, Amon Mpanju akimpigia debe Dk Magufuli eneo la Iwawa wilayani Makete
 Wananchi wakimsikiliza kwa makini Dk Magufuli mjini Makete
 Dk Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafuasi wa vyama vya upinzania waliovihama vyama vyao na kujiunga na CCM katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika  Iwawa, Makete leo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Mmoja wa wafuasi wa Chadema akiwa amesamama karibu na pikipiki yenye bendera ya chama hicho huku akimsikiliza kwa makini Dk Magufuli akijinadi katika Kijiji cha Kenja, wilayani Makete leo.
 Mfuasi wa Chadema (kulia) akishangilia baada ya kumsikia Dk Magufuli akitangaza kwamba akichaguliwa kuwa urais watoto watakuwa nasoma bure kuanzia darasa  la kwanza hadi kidato cha nne. Kutano huo ulifanyika katika Kijiji cha Kenja wilayani Makete baada ya msafara kuzuiwa wananchi katika eneo hilo wakiwa na hamu ya kusikiliza sera zake.
 Baadhi ya wananchi katika Kijiji cha Kenja wakimsikiliza Dk Magufuli huku wakiwa na mabango yenye picha za mgombea huyo wa urais wa CCM
 Dk Magufuli akisisitiza jambo katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Kenja wilayani Makete
 Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM,  William Lukuvi akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula katika mkutano wa kampeni wilayani Wangi ng'ombe, Mkoa wa Njombe leo
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Pindi Chana akihutubia katika kutano wa kampeni wa kumnadi Dk Magufuli wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe leo

 Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, Philip Mangula akisalimiana na Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli katika mkutano wa hadhara wa kampeni wilayani Wanging'ombe, mkoani Njombe
 Wananchi wa Kijiji cha Igagala wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali walipokuwa wakimlaki Dk Magufuli, wilayani Wanging'ombe, Njombe
 Dk Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Igagala, wilayani Wanging'ombe
 Wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa CCM mjini Njombe
Msanii Cgegge akitumbuiza katika mkutano wa kampeni za CCM kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe leo
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment