KANYAGA-TWENDE YA MAMA SAMIA YAMALIZIKA SINGIDA NA KUANZA DODOMA

 Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais ka tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akitoka Singida mjini kwenda Dodoma, kupitia Ikungi na Manyoni kufanya mikutano ya kampeni leo.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimsalimia Mkuu wa wilaya mpya ya Ikungi, Gishuli Charles, alipowasili eneo la Makyungu, kufanya mkutano wa kampeni katika jimbo la Singida Kaskazini lililopo katika wilaya hiyo ya Ikungi. Kushoto ni Katibu wa CCM, Ikungi, Aluu Sagamba.
 Wananchi wakimshangilia Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipowasili eneo la Makyungu kuhutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Singida Kaskazini, wilayani Ikungi.
 Wananchi wakiwa wamefurika kwenye mkutano huo wa Makyungu jimbo la Singida Kaskazini
 Mkuu wa mkoa wa Singida Parseko Kone akimsalimia Mkuu wa wilaya mpya ya Ikungi
 Kada wa CCM aliyeko katika kampeni za Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM akionyesha furaha kutokana na mambo kwenda vizuri katika mkutano wa kampeni wa Makyungu,jimbo la Singida Kaskazini
 Eti, CCM haina vijana! kwani hawa ni Wazee?
 Mzee Maarufu kwa jina la Mzee Jeuri aliyekuwa Kada wa Chadema, akizungumza baada ya kutangaza kuhamia CCM kwenye mkutano huo wa Makyungu
 Mzee jeuri akisalimiana na mgombea mwenza wa Urais Mama Samia Suluhu Hassan baada ya kuichana Chadema jukwaani, akisema kuwa chama hicho kimeua upinzania nchini kwa kumkaribisha Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa tuhuma za ufisadi, Edward Lowassa ambaye sasa ndiye mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema.
 Wananchi wakizidi kushamiri kwenye mkutano huo
 Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi akiwa amewabeba watoto Hussein na Hassan waliokuwa kwenye mkutan wa kampeni wa mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia kwenye eneo la Makyungu, Ikungi
 Mgombea Ubunge wa jimbo la Singida Kaskazini, Jonathan Njau akisalimia wananchi alipotambulishwa kwenye mkutano huo wa Makyungu.
 Mgombea Ubunge wa jimbo la Singida Kaskazini, Jonathan Njau akiomba kura kwa wananchi alipotambulishwa kwenye mkutano huo wa Makyungu
 Wananchi wakisikiliza Katibu Mkuu wa UWT, AminaMakilagi wakati akimkaribisha Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, MamaSamia kwenye mkutano huo wa makyungu
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akihutubia wananchi kwenye mkutano huo wa Makyungu, Ikungi mkoani Singida
 Mwandishi wa habari nguri wa TBC, Emmanuel Amas akiwa kazini wakati msafara ukielekea Dodoma baada ya kumalizika mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais Mama Samia
 Masafara wa Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan ukienda Manyoni kupiga mkutano mwingine wa kampeni
 Wananchi wakiwa kwenye mnara wa kumbukumbu, kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Manyoni, kumsubiri Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassani akiwasili kuhutubia mkutano wa kampeni kwenye Ofisi ya CCM Manyoni
  Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassani akiwasili kuhutubia mkutano wa kampeni kwenye Ofisi ya CCM Manyoni
 Mbunge wa Manyoni Mashariki, John Chiligati, akimuombea kura Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli, katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya CCM wilaya ya Manyoni
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, akihutubia mkutnao wa kampeni kwenye Ofisi ya CCM, Manyoni
BAHI-DODOMA
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akiwasili kwenye Uwanja wa mkutano wa kampeni, katika jimbo la Bahi mkoani Dodoma
 Wananchi wakiwa katika shamrashamra kumpokea Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia alipowasili jimbo la Bahi kuhutubia mkutano wa kampeni
 Mama Samia akiagana na baadhi ya viongozi wa CCM wa mkoa wa Singida waliomsingiza hadi Bahi mkoani Dodoma.
 Mgombea Mwenza wa Uras kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa CCm mkoa wa Singida waliomsindikiza hadi Bahi Dodoma 
 Wananchi waliofurika kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Bahi mkoani Dodoma
 Baadhi ya viongozi waliopo kwenye msafara wa mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni jimbo la Bahi mkoani Dodoma
 Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Singida, Diana Chilolo akimuombea kura Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Bahi mkoani Dodoma
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu, akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika jimbo la Bahi mkoani Dodoma.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akimnadi mgombea Ubunge, wa Bahi Omari Badwel, mkutano wa kampeni uliofanyika leo kaika jimbo la Bahi mkoani Dodoma leo. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO).
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment