KONGAMANO LA VIJANA MKOANI MBEYA WAKATI WA KUAZIMISHA SIKU YA VIJANA DUNIANI.

 Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Vijana Halmashauri jiji la Mbeya  Onah Temu akitoa hotuba katika siku ya Vijana Duniani ambayo kwa Mkoa wa Mbeya ilifanyikia Ukumbi wa Chuo kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya.
 Maandamano kuelekea katika Ukumbi ambapo vijana wanakutana kwa ajili ya Sherehe yao
 Mratibu wa Mradi wa Restless Fadhiri Mtanga akitoa mada kuhusu Maendeleo ya Vijana 
 Wakili Stephen John akiwashauri vijana kuto tumika na wanasiasa
 Muwezeshaji wa Sherehe hiyo ya Vijana  Mwadawa Mbando akiendelea kutoa utaratibu
 Vijana wakisikiliza kwa makini watoa mada kaika sherehe hiyo iliyofanyika ukumbi wa Mzumbe Mbeya
 Mmoja wa vijana kulia akipokea zawadi baada ya kupokea zawadi
 William Otuku akitoa Maada kuhusu afya ya Uzazi kwa vijana

 Picha ya pamoja 

KATIKA maadhimisho ya siku ya Vijana duniani yaliyofanyika Kimkoa katika ukumbi wa Chuo kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya, Vijana wamekumbushwa kuhusiana na afya ya uzazi kwa vijana pamoja na maendeleo yao.

Aidha katika kongamano hilo ambalo liliandaliwa na mashirika binafsi ya Restless Developmentna Young & alive initiative ambalo lilihudhuriwa na Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu na shule za Sekondari za Jiji la Mbeya.

Akizungumza katika kongamano hilo mwakilishi wa Shirika la Young & Alive Initiative, William Otuku, alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuwakumbusha vijana kuhusiana na maswala yanayohusu afya ya uzazi kwa vijana ili waweze kuwa na uwezo wa kushiriki shughuli za maendeleo wakiwa salama.

Aliongeza kuwa kauli mbiu ya siku hiyo ni kuhakikisha vijana wanashirikishwa na kuhusishwa  katika kupanga maamuzi mbali mbali hivyo hayo yote yanaweza kutimia endapo wataelimishwa kuhusiana na afya ya Uzazi ili waliomashuleni waendelee kufanya vizuri na kusaidia kutoa elimu kwa ambao hawako mashuleni.

“Vijana tunawapa elimuya afya  ya uzazi ili waweze kuwa imara katika kushiriki shughuli za maendeleo za kijamii pamoja na kuwaepusha na vitendo ambavyo vitaweza kuwaondolea katika hatari ya kupata magonjwa yanayoweza kuepukika” alisema Otuku.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa  Shirika la Restless Development,Fadhili Mtanga, alisema lengo la kongamano hilo ni kujadiliana kwa pamoja kuhusiana na changamoto ambazo zinawakabili vijana pamoja na kubadilishana mawazo juu ya kuweza kutatua na kukabiliana na vikwazo vya maendeleo kwa vijana.

Alisema lengo la kuwahusisha wanafunzi ni kutokana na kuwa na kundi kubwa la vijana wanaoanzia umri kati ya miaka 15 hadi 35 ambao ni kundi kubwa katika jamii hivyo ni rahisi kwao kupeleka mabadiliko kwa wananchi wengine ambao hawakubahatika kuhudhuria kongamano hilo.

“Sisi tumewalenga zaidi vijana ambao ni wanafunzi kwa sababu tunaamini wanakubalika kaika jamii na nirahisi kwao kutoa elimu ambayo iaweza kuwafikia wahusika kwa haraka zaidi” alisema Mtanga.

Naye Mgeni rasmi katika Kongamano hilo, Afisa Vijana wa Jiji la Mbeya, Ona Temu kutoka Ofisi ya Maendeleo ya Jamii Jiji la Mbeya, alipongeza kwa wadau kujitokeza na kuandaa kongamano hilo kwa kutambua mchango wa vijana katika jamii.

Alisema vijana wanapaswa kuutumia vizuri umri kati ya miaka 18 hadi 40 kwa kujenga na kutafuta uchumi ili kipindi cha miaka 40 hadi 60 anabaki kuwa msimamizi wa shughuli ambazo alizifanyia kazi kipindi cha ujana wake.

Aliongeza kuwa kipindi cha umri wa zaidi ya miaka 60 ni muda wa kufaidi matunda na kupumzika kwani utakuwa tayari umeshafanya kazi ya kutafuta na kuzisimamia vizuri kwa malengo makubwa.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment