MAFISADI WAHAHA KUMZUIA NAPE MTAMA


Ikiwa imebaki siku moja kufanyika kwa kura za maoni Ubunge wa Jimbo la Mtama ,kumekuwa na michezo ya kumchafua kisiasa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye ni mmoja wa wagombea wenye nguvu kubwa kwa jimbo la Mtama.
Huku hujuma hizo zikihusishwa na mikakati ya mafisadi kumzuia Nape, ambaye amekuwa mwiba mkali sana kwa mafisadi kwa miaka sasa, ametajwa aliyekuwa akitafuta kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM ambaye jina lake lilikatwa katika hatua za awali kuhusika na njama hizo chafu.
Taarifa zilizosambazwa jioni hii kwenye mitandao mbalimbali zilidai Nape amehojiwa na Takukuru Lindi kwa Masaa matano wakati haikuwa kweli.
Kamanda wa PCCB mkoa wa Lindi S. Chami amethibitisha kuwa Nape Nnauye alikuwa ametoa pesa benki kwa ajili ya malipo ya mawakala na si wajumbe kama ilivyovumishwa.
"
CORRECTION: After questioning, it turned out that the money Nape Nnauye withdrew  was for agents, not delegates, Lindi  PCCB  boss S. Chami clarifies Friday."
Nape amesema anajua mafisadi wanahaha kumchafua hata kufikia hatua ya kutumia baadhi ya watumishi wa serikali na mitandao ya kijamii lakini hawatofanikiwa.
" Najua wanaogopa nikiingia bungeni itakuwa kiama chao, sasa wanahaha kunizuia. Wametumia pesa na ghiliba za kila namna wanashindwa na watashindwa vibaya kesho. Mungu mkubwa" alikaririwa Nape
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment