PATO LA TAIFA ROBO YA KWANZA YA MWAKA 2015 LAFIKIA SHILINGI TRILIONI 21.9

Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morrice Oyuke (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu pato la taifa robo ya kwanza ya mwaka kuanzia Januari hadi machi 2015. Kushoto ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa.
Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morrice Oyuke (kulia), akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Wapiga picha za habari na wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale


MATOKEA ya Takwimu za Pato la Taifa kwa robo mwaka bei za miaka inayohusika yameonyesha kuwa thamni ya pato la taifa katika kipindi cha robo ya kwanza ya 2015 ilikuwa ni sh. 21.9 trilioni ikilinganishwa na sh. 18.6 trilioni ya robo mwaka ya kwanza mwaka 2014.


Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morrice Oyuke, wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu pato la taifa robo ya kwanza ya mwaka kuanzia Januari hadi machi 2015.


Oyuke alisema pato la Taifa kwa bei za mwaka 2007 katika kipindi cha robo mwaka ya kwanza linaonyesha kuwa jumla ya thamani ya shilingi 10.6 trilioni kwa mwaka 2015 ikilinganishwa na sh.trilioni 9.9 trilioni katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2014.


"Hii inamanisha kuwa pato la taifa liliongezeka kwa kasi ya asilimia 6.5 katika kipindi cha robo ya kwanza mwaka 202015 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 8.6 katika kipindi kama hicho mwaka 2014" alisema Oyuke


Oyuke alisema kuwa shughuli za kiuchumi za kilimo na mifugo zilikuwa kwa kasi ya asilimia 2.6 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2015 ikilinganishwa na kasi ya ukuaji wa asilimia 3.4 katika kipindi kama hicho mwaka 2014.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)


Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment