RAIS KIKWETE AZINDUA BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO TANZANIA (TADB) DAR ES SALAAM

 Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akihutubia wakati akizindua Benki ya Maendeleo ya Kilimo Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira. Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa benki hiyo. Uzinduzi wa awamu ya pili wa benki hiyo utafanyika kesho kwenye maonyesho ya Nanenane kitaifa mkoani Lindi.
  Rais Jakaya Kikwete, akivuta pazia kuashiria uzinduzi wa benki hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Thomas Samkyi, akizungumza katika uzinduzi huo.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo , Rosebud Violet Kurwijila, akizungumza katika uzinduzi huo.
  Rais Jakaya Kikwete (katikati), na viongozi wengine wakipiga makofi wakati wa uzinduzi wa benki hiyo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Thomas Samkyi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo , Rosebud Violet Kurwijila,Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira. 
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Rais Kikwete (katikati), akiwa na viongozi wa benki hiyo.Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Thomas Samkyi, Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo , Rosebud Violet Kurwijila. 
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment