TAARIFA KWA UMMA, TAARIFA ZA UZUSHI ZILIZOENEA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU DKT. BILAL SI ZA KWELI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasikitika kuwepo kwa taarifa za uzushi ambazo zimesambaaa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ataongea na vyombo vya habari kuhusu msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.

Habari hizi si za kweli na tunaomba kuueleza umma wa Watanzania kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais, hausiki na taarifa hizo zilizoenea kwenye mitandao ya Kijamii na wala hajapanga tukio lolote la kukutana na waandishi wa habari na wala hana mpango wa kuzungumzia msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.

Aidha tunatumia nafasi hii kuwataka wale wote wenye tabia ya kuvumisha taarifa zisizo sahihi kwa maslahi yao waache kufanya hivyo kwa kuwa ni kosa kisheria. Tunawaomba waandishi wa habari kufuata taratibu za kazi na kutafuta taarifa sahihi kwenye vyombo vinavyohusika na kutambulika.

Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais
10/8/2015
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment