TAMASHA LA MUZIKI MNENE BAR KWA BAR KUENDELEA KIVINGINE

Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa kituo cha Redio cha EFM,  Denis Ssebo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habri Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu  kuendelea kufanyika kwa Tamasha la Muziki Bar kwa Bar baada ya kumalizika kwa tamasha hilo kwa awamu ya kwanza. Kulia ni Mtangazaji, Dina Marios.Na Dotto Mwaibale

KITUO cha Redio cha EFM kimeamua kuendelea kufanya tamasha la muziki Bar kwa Bar baada ya kumalizika kwa tamasha hilo kwa awamu ya kwanza.

Hayo yalibainishwa na Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa kituo hicho, Denis Ssebo wakati akizungumza na waandishi wa habri Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu tamasha hilo.

"Baada  ya kumalizika kwa Tamasha la musiku mnene Bar kwa bar awamu ya kwanza, na mashabiki kuomba Burudani hiyo iendelea tena Kituo chetu cha  Redio cha Efm kimekubali  ombi hilo na sasa tamasha hilo linarudi tena kwa kishindo likiwa  limeboreshwa kwakuongeza wigo wa kuwafikia watu wengi zaidi" alisema Ssebo.

Alisema Muziki mnene bar kwa bar awamu hii bila kuwasahamu wasikilizaji na mashabiki wa EFM katika wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala kwa umuhimu wake na Wilaya mpya katika mkoa wa Dar es salaam, Muziki mnene sasa utapelekwa pia katika mkoa wa Pwani.

Ssebo alitaja maeneo ambayo wanatakiwa kukaa tayari  kwa Muziki mnene bar kwa bar utakaoporomoshwa  na Madjs wakali wa Efm, ni pamoja na Kibaha, Mlandizi, Mkuranga, Bagamoyo, Kisarawe,  Kigamboni na maeneo mengine mengi kwa ajili ya kuhakikisha tunakonga nyoyo za mashabiki wetu.

Alisema Muziki Mnene bar kwa bar mwaka huu inatarajiwa kuanza rasmi Septemba 5 mwaka huu lakini katika kuelekea huko efm imeanza na muziki mnene bango katika sehemu yako ya biashara ambako bwana E anapita na ukiwa umeweka bango la EFM na unasikiliza matangazo yetu basi utapata kifurushi chenye zawadi kibao.

Aliongeza kuwa mwishoni kutakuwa na Tamasha kubwa la hitimisho ambalo litafanyika jijini Dar es salaam ambalo safari hii limeboreshwa na kuongezwa vionjo vingi sana.

“Ninawaomba wasikilizaji wetu wakae mkao wa kula maana tutawafikia na kuwamiminia Burudani ambayo pia itarushwa live kutoka eneo husika kupitia kituo chao cha 93.7 EFM. Njoo tuonane, tufahamiane na tuijenge Radio yetu efm ambayo kwetu Muziki unaongea”. alisema Ssebo.

Ssebo alipenda kutumia fursa hiyo kuwajulisha umma kwamba katika kuhakikisha wanaendelea kutoa burudani iliyobora zaidi kupitia vipindi vyao mbalimbali,sanjari na kuwa na watangazaji wenye ushawishi na uwezo mkubwa wame mtambulisha kwenu mtangazaji Dina Marios ambaye wengi uwezo wake mnaujua na sasa ameungana na wenzake  wenye uwezo mkubwa katika familia ya Efm. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com simu namba 0712-727062)
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment