WADHAMINI WA LIGI YA BODABODA KIPUNGUNI "B" MFUKO WA PENSHENI WA PSPF WAFUNGUA RASMI MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU


 
  Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Delphin Richard akizungumza na madereva bodaboda wa Kipunguni 'B' kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga
  Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa akizungumza na wananchi mbalimbali waliofanikiwa kuhudhuria ufunguzi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva bodaboda wakiume maeneo ya Kipunguni 'B' katika manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam
 Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma  akitoa maelezo ya kina kuhusu faida na huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari, ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga na kunufaika na huduma mbalimbali zilizo katika hifadhi ya jamii ya (PSPF), akiongea na madereva wa bodaboda wa Kipungunu 'B' wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva hao.
  Delphin Richard Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,  akisalimiana na muamuzi wa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Madereva wa Bodaboda wa Kipunguni 'B' ambapo mfuko wa PSPF imedhamini mashindano hayo. Katikati ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa.

 
 Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa akitambulishwa wachezaji
 Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliachi Remmy akisalimiana na wachezaji katika ufunguzi wa ligi ya madereva bodaboda.
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Delphin Richard akizungumza mmoja wa wazee kuhusu Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari, ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga na kunufaika na huduma mbalimbali zilizo katika hifadhi ya jamii ya (PSPF)
  Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma akimjazia fomu ya Uchangiaji wa Hiari mmoja wa madereva wa Bodaboda wa Kipunguni B wilaya ya Ilala jijini Dar mara baaada ya kupata elimu na kuridhia na huduma za mfuko huo.

 Madereva bodaboda wawana mwitikio mkubwa wa kujiunga na mfuko wa PSPF kupitia (PSS) kwakujaza fomu za Uchangiaji wa Hiari
 Afisa wa mfuko wa pensheni, Delphin Richard(kushoto) akimuonesha sehemu ya kuweka alama ya dole gumba mmoja wa madereva wakati wa ujazaji  fomu za Uchangiaji wa Hiari
 Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliachi Remmy(kulia) akiwajazia fomu za Uchangiaji wa Hiari mmoja wa madereva wa Bodaboda wa Kipunguni B wakati wa mashindano ya mpira wa miguu katika eneo la Kipunguni B 

Madereva bodaboda wa mtaa wa Kipunguni 'B' kata ya Kivule manispaa ya Ilala wameanzisha ligi  ya mpira wa miguu kwaajiri ya kuendeleza kujenga afya zao kwa michezo kwani michezo ni afya kwa wote, wakati wa ufunguzi huo wa ligi hiyo ya madereva bodaboda wadhamini wa ligi hiyo ambao ni Mfuko wa pensheni wa (PSPF)nao hawakuwa mbali kwaajiri ya kuwawezesha madereva hao kwa kipindi chote cha ligi hiyo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ligi hiyo mgeni rasmi ambaye ni mkaguzi msaidizi wa polisi kanda maalumu ya dare s salaam Josephat Sylvery Tirumanywa amewaasa madereva hao kuwa waweze kucheza kwa amani michezo yote na pia waweze kuwa ni miongoni mwa watu watakao jiunga na na mfuko wa (PSPF) ka kupitia (PSS) kwaajiri ya kuendelea kupata huduma zilizo bora na  zenye uhakika .

Pia Afisa masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Ismail Juma amesema wameamua kuungana na madeeva boda boda hao ili kuweza kuwapa elimu katika suala la kuwekeza na kufaidika na mafao mbalimbali yanayo tolewa na PSPF kwani Pindi watakapo jiunga na mfuko huo wataona matunda mengi hasa kutokana na kuwa ni watu ambao wanategemewa na familia zao hivyo kama Pspf wana mafao ambayo wataweza kujikwamua kama mafao ambayo wanaweza kuwasomesha watoto,vilevile fao la uzazi hata fau la nyumba pia ujiungapo na mfuko huu utafaidika na wala hauto jutia 

Naye Bw.Delphin Richard ambaye pia ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa (PSPF) amewasisitiza madereva kutii sheria za barabarani na pia kuweza kucheza ligi hiyo kwa amani maana wamepewa dhamana ya kuwasafirisha abiria kwa amani na upendo ,hivyo kati ya jeshi la polisi na madereva husaidiana kufanya kazi kwa umoja na hivyo kuweka mahusiano mazuri katika kufanikisha nchi yetu inajengwa na sisi watanzania kwa kuendeleza upendo na amani pindi tuwapo barabarani,aliongeza kwa kuwapa shukrani madereva ya kuweza kuchagua mfuko wa pensheni wa Pspf kuwa wadhamini wa michuano hiyo kwani PSPF ipo kwaajiri ya kila mmoja  na kuweza kuwaasa  waweze kuwahamasisha watu mbalimbali kuweza kujiunga na mfuko huo ili kuhakikisha mabadiliko ya wananchi mbalimbali yanatokea kimaisha ,elimu,afya na mengine mengi.

Mfuko wa pensheni wa PSPF unafuraha ya kuwa kwa sasa wananchi wanajua kile kilicho sahihi nakuongeza kuwa wananchi mbalimbali waweze kufika maeneo ya kipunguni B ilikuweza kushirikiana na madereva hao kwa kuwashangilia wakati ligi ikiwa inaendelea na ligi hiyo itakayo dumu kwa takibani wiki moja.


Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment