WASHIRIKI WA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE KUPITIA VIPODOZI WAHITIMU MAFUNZO

  Washiriki wa Manjano Dream-makers katika taasisi ya Manjano Foundation wamehitimu mitihani yao ya mwisho ya jinsi ya kupaka vipodozi (makeup). Kuanzia sasa, washiriki hao wanawake na wasichana 30 wanaianza safari yao ya mwaka mzima katika kujikita na ujasiriamali. Taasisi ya Manjano Foundation, ilianzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa programu ambayo itamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwezesha kujiongezea kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha yake.
 Kundi hili la washiriki waliohitimu mafunzo mbali mbali linabeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, ukiwa ni mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano. 
 
Mradi huu uliandikwa na kuandaliwa na kampuni ya SSC Consulting wakiwa ndio washauri wakuu wa mradi huu, hasa katika kuandaa Utaratibu na mipango yote ya mafunzo ya biashara na ujasiriamali. Mradi huu unadhaminiwa na kampuni ya Shear illusions kwa lengo la kuwajengea uwezo wanwake wa Kitanzania Kupitia Bidhaa bidhaa za Vipodozi vya LuvTouch Manjano kujisimamia na kujikita vizuri kwenye Biashara ya Vipodozi na kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara kwa lengo la Kumjengea uwezo Mwanamke wa Kitanzania.  Kila mshiriki amepewa mtaji wa bidhaa za LuvTouch Manjano, vitendea kazi kumuwezesha kuwapodoa wateja, mafunzo ya biashara na ujasiriamali na pia atapewa Business Coach na Mentor (Dada mshauri) ili kumuongoza katika safari hii ya mwaka mzima katika kujikita kwenye ujasiriamali. Tunawatakia kila la kheri kizazi kipya hiki cha wajasiriamali kina mama. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser Muasisi wa Mradi  aliouanzisha kuwejengea Uwezo wanawake Kwenye  Ujasiriamali.Mafunzo  Chini ya Taasisi ya  Manjano Foundation.Lengo la Mradi huo ni kuwajengea Uwezo wanwake wa Kitanzania Kupitia Bidhaa bidhaa za Vipodozi vya Luv touch Manjano kujisimamia na Kujikita Vizuri kwenye Biashara ya Vipodozi na kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara kwa lengo la Kumjengea uwezo Mwanamke wa Kitanzania.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment