Waziri wa Fedha Zanzibar Omar Yussuf Afanya ziara kutembelea Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani

Mnara ya Kumbukumbu ya Maspinduzi Zanzibar ukiwa katika hatua za mwisho ya ujenzi wakeMnara huo una urefu wa mita 35 kwenda juu, unaojengwa kwa mradi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF. ulioko katika viwanja vya michezani Zanzibar. 
Mkurugenzi wa Mfuko wa Jamii Zanzibar (ZSSF) Ndg. Adulwakil Haji Hafidh, akitowa maelezo ya ujenzi wa Mnara huo wakati wa ziara ya Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee alipofika kuutembelea Mnara huo kujionea kazi za umaliziaji wa ufungaji wa vifaa kwa hatua za mwisho za ujenzi wake, Wakiwa katika moja gorofa ya juu ambayo itakuwa ni mgahawa wa aina yake utakuwa unazunguka kuangalia mandhari ya eneo hilo.
Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe. Omar Yussuf Mzee akizungumza na Wajumbe swa Bodi ya Udhamini wa ZSSF na Uongozi wa Mfuko huo kushoto Mwenyekiti wa Bodi ya ZSSF Dk. Suleiman Rashid akimsikiliza Waziri Omar akitowa maelekezo kwa Wajumbe wa Bodi jinsi ya kuuendesha Mnara huo kibiashara,
Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee, akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya ZSSF na Uongozi wa ZSSF wakati wa ziara yake kutembelea kuona maendeleo ya mwisho ya ujenzi wa Mnara huo wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Zanzibar.  
Mkurugenzi Muendeshaji wa ZSSF Ndg Abdulwakil Haji Hafidh akimtembeza Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee alipofika kuangalia ujenzi huo ukiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake unaofanywa na Kampuni ya Ujenzi kutoka China.
Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee, Mkurugenzi Muendeshaji wa ZSSF Ndg, Abdulwakili Haji Hafidha na Wajumbe wa Bodi ya ZSSF wakitembelea Ujenzi wa Mnara huo wakati wa ziara ya Waziri wa Fedha.  
Waziri wa Fedha akitembelea mnara huo akiwa katika sehemu itakayokuwa na ATM za Benki ya Watu wa Zanzibar itatoa huduma za kibenki kupitia mashine za ATM kwa Wananchi wanaofika katika Mnara huo.

Waziri Yussuf akitembelea eneo la mnara huo wakati wa ziara yake. akiwa na Wajumbe wa Bodi na Uongozi wa ZSSF Zanzibar.
Sehemu ya Chumba cha Picha za kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar ilioko katika Mnara huo sehemu ya chini ambayo itakuwa na mapicha mabilimbili yanayoonesha historia ya Zanzibar na chuma cha sinema ya kumbukumbu ya Zanzibar.  
Sehemu ya Mgahawa katika Mnara huo ambayo inazunguka kuweza kuangali sehemu ya mandhari ya maeneo hayo ukiwa unapata huduma ya Mgahawa. 
Wajumbe wa Bodi ya ZSSF na Uongozi wakiwa sehemu ya juu ya Mnara huo wakati wa ziara ya Waziri wa Fedha Zanzibar, alipotembelea mnara huo.
Mjumbe wa Bodi ya ZSSF Ndg Mohammed Baloo akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya ZSSF wakati wa ziara ya Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee. 
Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee akiwa katika picha ya opamoja na Viongozi wa Bodi na Uongozi wa ZSSF. baada ya zuiara yake kutembelea Mnara wa Kumbuykumbu ya Mapinduzi Zanzibar.
Share on Google Plus

About Jestina George

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment