Mhe.Eng.Hamad Masauni Afungua Mafunzo ya Vijana wa TUEPO Kuwajengea Uwezo Vijana Kujiajiri Wenyewe

Mmoja wa Kijana Wasio na Ajira Tanzania akisoma Quran wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Siku mbili ya kuwajengea Uwezo Vijana wa Jumuiya ya Watanzania Wasuio na Ajira Tanzania (TUEPO) yanayofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Zanzibar.
Katibu wa Jumuiya ya TUEPO Muzna Ibarahim akitowa maelezo ya mafunzo hayo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin Mhe Hamad Masauni kuyafungua mafunzo hayo ya siku mbili yanayowajumuisha Vijana wasio na Ajira kuwajengea Uwezo wa kujiajiri.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Eng Hamad Masauni akifungua m,afunzo ya Vijana Wasio na Ajira yalioandaliwa na Jumuiya ya Watanzania Wasio na Ajira Tanzania (TUEPO) mafunzo hayo yanafanyika katika ukmbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar.
Mhe Eng Hamad Masauni akitowa nasaha zake kwa Vijana wanaohudhuria mafunzo ya siku mbili ya Kuwajengea Uwezo wa Kujiajiri yalioandaliwa na Jumuiya ya Watanzania Wasio na Ajira Tanzania 
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mhe Eng, Hamad Masauni wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Vijana washiriki katika mafunzo ya Vijana Wasio na Ajira wakifuatilia ufunguzi wa mafunzo hayo uliofanywa na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe Eng. Hamad Masauni. mafunzo hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Watanzania Wasio na Ajira Tanzania.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Wasio na Ajira Tanzania Mwalim Ussi akitowa maelezo ya mafunzo hayo wakati wa ufunguzi na kuelezea malengo ya Jumuiya hiyo kwa Vijana kutowa mafunzo ili kuweza kujiajiri katika sekta mbalimbali Tanzania.
Mkufunzi wa Mafunzo ya Jumuiya ya Watanzania Wasio na Ajira Ndg Abel Kipapi, akitowa Mada kuhusiana na Ubunifu katika Kazi kwa Vijana Kujiajiri wakati wa mafunzo hayo ya Siku Mbili yaliowashirikisha Vijana Wasio na Ajira Tanzania kuweza kujiajiri wenyewe.  
Baadhi ya Vijana Wasio na Ajira wakifuatilia Mada iliokuwa ikiwasilishwa wakati wa mafunzo hayo

Vijana wakiwa makini wakifuatilia mafunzo hayo ili kuweza kupata ujuzi wa kujiajiri wenyewe baada ya kupata mafunzo hayo yaliotolewa na Jumuiya ya Watanzania Wasio na Ajira Tanzania.
  Mhe Eng Hamad Masauni akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Mafunzo hayo ya TUEPO
Mhe Hamad Masauni akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo baada ya ufunguzi wake. Picha na Zanzinews.com  
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment