MHESHIMIWA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA AFUNGUA MKUTANO WA WATANZANIA (DIASPORA BUSINESS CONVENTION 2015) BIRMINGHAM NCHINI UINGEREZA


Mheshimiwa Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula, Mheshimiwa Balozi wa Tanzania, Uingereza, Peter Kallaghe, Mheshimiwa Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi Zanzibar, Bwana Salum Maulid, Mwenyekiti wa Watanzania waishio Birmingham, Prince Katega na Mwakilishi wa Watanzania waishio Birmingham katika Ufunguzi wa Mkutano wa Watanzania waishio nchini Uingereza

Mtanzania akiimba Wimbo wa Taifa kuashiria Ufunguzi wa Mkutano wa Tanzania Diaspora Business Convention 2015. Mkutano unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Bingley Hall katika jiji la Birmingham, Uingereza


Dada Suzan Mzee, Mshauri wa Diaspora katika Ofisi ya Waziri Mkuu, akiongea machache na Watanzania wanaoshiriki Mkutano wa Tanzania Diaspora Business Convention 2015
Baadhi wa Watanzania wanaoshiriki Mkutano wa Watanzania waishio nchini Uingereza

Baadhi wa Watanzania wanaoshiriki Mkutano wa Watanzania waishio nchini Uingereza
Baadhi wa Watanzania wanaoshiriki Mkutano wa Watanzania waishio nchini Uingereza
MC wa Mkutano, akifungua Mkutano wa Watanzania waishio nchini Uingereza

Washiriki wa Mkutano wa Tanzania Business Convention 2015, unaendelea leo siku ya Jumamosi 5/9/2015
Baadhi wa Watanzania wanaoshiriki Mkutano wa Tanzania Diaspora Business Convention 2015. Mkutano ambao unaendelea hivi sasa siku ya Jumamosi katika Ukumbi wa Mikutano wa Bingley Hall, katika Mji wa Birmingham nchini Uingereza


Watanzania wakifuatilia kwa makini mkutano wa Watanzania waishio nchini Uingereza
Balozi wa Tanzania, Uingereza Mhe. Peter Kallaghe pamoja na Mr. Katega (Mwenyekiti wa Tanzania Birmingham), wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa mitambo ya kufua umeme asilia (Renewable energy), katika Ukumbi wa Bingley Hall - Birmingham, wakati wa Mkutano wa Tanzania Diaspora Business Convention ambao unaendelea tena leo siku ya Jumamosi 05/09/2015
Bwana Amos Msanjila (Afisa Ubalozi wa Tanzania, Uingereza - kushoto), Dada Elizabeth Rwitunga - Afisa Wizara mambo ya Nje, Bwana Alto Ernest Chaula na Bwana Abdallah Makunja -Maofisa Wizara ya Mambo ya ndani, Tanzania (Uhamiaji) na Dada Asma Msanjila.
Mheshimiwa Balozi wa Tanzania, Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe, akipata maelezo kutoka kwa Mshiriki wa upande wa Sanaa za Mikono kutoka Tanzania, katika Ukumbi huo wa Mkutano ambapo Tanzania Diaspora Business Convention unaendelea tena leo.

Baadhi wa Washiriki katika Mkutano wa Diaspora Business Convention unafanyika kwa mwaka huu 2015


Washiriki katika Mkutano wa Diaspora Business Convention mwaka 2015, katika mji wa Birmingham
Bwana Amos Msanjila (Afisa Ubalozi wa Tanzania, Uingereza), akimkaribisha Bwana Salum Maulid - Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi, Zanzibar, kwenye Ukumbi wa Mikutano, ambapo Mkutano wa Watanzania waishio Uingereza unafanyika kwa Mwaka huu wa 2015.

Dada Elizabeth Rwitunga, akisalimiana na Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi, Zanzibar - Bwana Salum Maulid
Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi, Bwana Salum, akisalimiana na Watanzania mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Mikutano
Baadhi ya Watanzania wakipata Vinywaji kabla ya Ufunguzi wa Mkutano wa Tanzania Diaspora Business Convention katika Ukumbi wa Bingley Hall - Birmingham
Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi, Bwana Salum Maulid, akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula katika Ukumbi wa Mikutano wa Bingley Hall - Birmingham

Mheshimiwa Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula, akisalimiana na Watanzania mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Mikutano, ambao Mkutano wa Watanzania waishio Uingereza unafanyika kwa Mwaka huu wa 2015


Mheshimiwa Katibu Mkuu, akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Washiriki wa Mkutano huo.

Mheshimiwa Katibu Mkuu, akiongea na Dada Hamida kutoka Manchester, akionyesha kazi zake za Sanaa ya Mikono, ambayo amekuwa akishughulika nayo kila siku hapa nchini Uingereza

Mheshimiwa Katibu Mkuu akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa Kampuni ya kutengeneza Vigae na Matofali. Kampuni hiyo ambayo inatengeneza huduma hizo kutokana na njia ya utunzaji wa mazingira
Katibu Mkuu, Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi, Bwana Salum Maulid, Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe, mama Joyce Kallaghe, wakiwa na mwakilishi wa Kampuni ambayo inatengeza Mitambo ya kusafishia Maji taka (machafu) na kuwa safi na salama kwa matumizi ya Binadamu na Viumbe wengine. Mashine hizo ambazo ni nafuu, zinaweza kutumika sehemu mbalimbali hapa Tanzania kwa kusafishia maji

Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania, Mhe. Peter Kallaghe, Bwana Price Katega na Mama Joyce Kallaghe, wakipata maelezo kutoka kwa Mwakilishi wa Bandari, Tanzania, ambao pia wameshiriki kwenye Mkutano wa Watanzania waishio Uingereza mbao unaendelea leo hii siku ya Jumamosi tarehe 5/9/2015 katika Ukumbi wa Bingley Hall - katika mji wa Birmingham, Uingereza.
Mheshimiwa Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi Zanzibar, Mama Joyce Kallaghe na Bwana Price Katega wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa washiriki wa kazi za Mikono kutoka Tanzania
Mwakilishi katika Mkutano wa Watanzania waishio nchini Uingereza, akitoa maelezo ya Huduma zao kwa Mheshimiwa Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula
Mheshimiwa Katibu Mkuu, akiangalia kazi za mikono kutoka kwa mmoja wa Washiriki katika Mkutano huo wa Watanzania
Mheshimiwa Katibu Mkuu, Mama Joice Kallaghe na Bwana Price Katega wakipata maelezo kutoka kwa mwakilishi wa Benki ya Santander ya Uingereza
 Mheshimiwa Katibu Mkuu akisalimiana na kuongea na baadhi wa Watanzania waliohudhuria Mkutano wa Watanzania waishio nchini Uingereza
Mheshimiwa Katibu Mkuu akisalimiana na Mshauri wa Mambo ya Diaspora katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Dada Suzan Mzee pamoja na dada Joyce kutoka Manchester

Mheshimiwa Katibu Mkuu, akiongea na baadhi ya Watanzania walioshiriki kwenye Mkutano wa Watanzania waishio nchini Uingereza  

Baadhi ya Watanzania wanaoshiriki katika Mkutano wa Tanzania Diaspora Business Convention katika Ukumbi wa Bingley Hall, Birmingham, mkutano ambao unaendelea tena leo hii siku ya Jumamosi baada ya Ufunguzi rasmi hapo jana.

Mr. Rashid Dilunga
ICT Manager


Tanzania Trade Centre
Tanzania High Commission
3 Stratford Place
London W1C 1AS
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment