MWIGULU NCHEMBA NI HALF-MAN HALF-MACHINE,AITEKA MBEYA KWA SIKU MOJA

Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi wa Mji wa Tunduma mapema asubuhi ya leo alipokwenda kuomba kura za Rais,Ubunge na Madiwani wa Chama cha Mapinduzi."Watanzania wenzangu mnaoishi hapa Tunduma,Hakuna chama cha siasa chenye thamani kuliko UHAI wa Mwanadamu,Nawaombeni sana muache tabia za kupigana na kuuana kwasababu ya vyama vya siasa.Nyie wananchi mnagombana kwa sababu ya siasa,Hivi ni lini mmeona sisi viongozi wa vyama vya siasa tunapigana??"Mwigulu NchembaWananchi wa Tunduma wakishangilia hoja za Mwigulu Nchemba kuhusu Uadui wa vyama vya siasa na Uongozi wanaokwenda kuuchagua.Furaha ya WanaCCM wanapothibitishiwa Usalama wao wakati wa kwenda kupiga kura hapo October 25."CCM tumefanya hesabu kwenye Uchaguzi huu na hesabu imekubali,Magufuli anakwenda kushinda Uchaguzi huu.Mgombea wa CCM hadi sasa anawazidi wagombea wengine kwa Uadilifu,Ubora wa sera zake,rekodi yake ya Uchapakazi lakini ni Mzalendo kwa Taifa lake"Mwigulu akizungumza na wananchi wa Tunduma hii leo.Mwigulu akimnadi Mgombea Ubunge Ndg.Frank wa Chama cha Mapinduzi wakati wa mkutano huo."Twendeni tukaichague CCM,Chama chenye Dira ya maendeleo ya kweli wa Watanzania,hao wengine wangekuwa wanmabadiliko wangeyafanya wakati walipokuwa serikalini,Hivi sasa hawana nafasi tena"Umati wa Wananchi wa Mji wa Tunduma wakiendelea kusikiliza Mkutano wa Mwigulu Nchemba mapema hii leo asubuhi.Kura za wazi wa Magufuli kutoka kwa Wananchi wa Tunduma walipoulizwa na Mwigulu Nchemba watakao mpigia kura Magufuli wainue mikono yao.Wananchi wakifuatilia mkutano kwa makini tayari kwa kufanya maamuzi ya kuipigia kura CCM."Serikali imejipanga kweli kweli kuhakikisha Usalama wa Watanzania utatamalaki kipindi chote cha Uchaguzi,Nendeni mkapige kura".Makada wa tiifu wa Chama cha Mapinduzi wakikutana hii leo Kyela.Ni Dr.Harrison Mwakyembe na Mwigulu Nchemba.Hisia za Wanakyela wanapoambiwa Nchi nzima wanaimba Magufuli,Hivyo hakuna shaka juu ya Ushindi wake."Nimekuja kuwashauli kama ndugu zangu,Leo hii Tanzania na Dunia yote inamjua Mwakyembe kwa Uchapa kazi wake,Mwakyembe anastahili kupigiwa kura ya NDIYO na sio kupingwa,Ametekeleza ilani ya CCM ndani ya jimbo kwa kiasi kikubwa,Muungeni mkono akamalizie alipoishia"Mwigulu."Twende na Magufuli,tunataka kazi tu"Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa kata ya Nzovwe jioni ya leo."Vijana wenzangu wa Uyole,Maendeleo hayaji kwa kupiga Rami deki ili mtu ambaye Upinzani kwa miaka Zaidi ya 10 walikuwa wanamuita Mwizi,Maendeleo yanakuja kwa mipango.Msipandikizwe chuki juu ya CCM,wakati watendaji wa serikali hawaajiliwi kwa kadi za CCM na wengine wapo serikalini hawana hata urafiki na CCM.Hivyo basi tumewaletea Magufuli abadilishe utendaji serikalini na sio vyama vya siasa".Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa kata ya Uyole hii leo Jioni.WanaCCM wakishangilia hoja za Mwigulu Nchemba.Wananchi wa Uyole(Junction)wakimsindikiza Mwigulu Nchemba kwenda kupanda Gari mara baada ya Mkutano wa hadhara wa kumuombea kura Magufuli,Diwani na Mbunge wa CCM.
Picha na Sanga Festo Jr.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment