Rais Kikwete akabidhi vitabu Chuo Cha ulinzi cha Taifa(National Defence College)

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange vitabu kwaajili ya Chuo Cha ulinzi cha Taifa National Defence College(NDC) katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho cha NDC Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue,Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange,Mkuu wa Chuo Cha NDC Meja Jenerali Gaudence Milanzi wakiangali baadhi ya vitabu ambavyo Rais ameviakbidhi kwaajili ya matumizi ya Chuo hicho
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue(watatu kushoto),Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange,(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi Cha Taifa(NDC) Meja Jenerali Gaudence Milanzi(kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania muda mfupi baada ya Rais Kikwete kukabidhi vitabu kwaajili ya National Defence College) katika hafla iliyofanyika ikulu jijijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy MRO)

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo Jumatatu Oktoba 26, 2015, amelikabidhi Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vitabu kwa ajili ya vyuo vyake na maktaba zake, ikiwa ni mara ya tano kwa Rais Kikwete kulikabidhi Jeshi hilo vitabu wakati wa uongozi wake.

Vitabu hivyo 384 vilivyokabidhiwa leo vitatumiwa na Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha National Defence College (NDC) na wanafunzi wanaosoma katika Chuo hicho chenye hadhi ya kimataifa.

Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Gaudence Milanzi amehudhuria sherehe ya makabidhiano ya vitabu hivyo ambavyo Rais Kikwete amevikabidhi kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange katika sherehe fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Hiyo ni mara tano kwa Rais Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu kukabidhi vitabu kwa JWTZ katika azma yake ya kuboresha vyuo na maktaba ya vyuo hivyo vya Jeshi. Mpaka sasa, Rais Kikwete amekwisha kabidhi vitabu 3,136 kwa Jeshi.

Rais Kikwete aliahidi kulinunulia na kulikabidhi Jeshi vitabu (titles) mbali mbali 503 na kufuatia makabidhiano ya leo, sasa vimebakia vitabu (titles) 27 ambavyo navyo tayari vimenunuliwa na vinasubiriwa kusafirishwa kuletwa nchini kutoka vilikonunuliwa.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
26 Oktoba, 2015
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment