UNESCO KUENDELEZA UTAMADUNI WA KUZISAIDIA REDIO JAMII

IMG_4940
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Utawala na Fedha), Bw. Liberat Mfumukeko alipowasili katika chumba maalum cha wageni kabla ya kuelekea kwenye ufunguzi wa kongamano la siku tatu la Mtandao wa Redio za Jamii katika nchi za Afrika Mashariki (EACOMNET) linalolenga kujadili namna ya kuziwezesha redio hizo kujiendesha katika mipango endelevu kwa kuwa na mipango sahihi ya kifedha bila kutegemea fedha kutoka kwa wafadhili ili ziweze kutoa mchango unaokusudiwa kwa wananchi linaloendelea katika makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Na Modewjiblog team, Arusha

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limeonyesha nia yake ya kuendeleza utamaduni wa kuzisaidia redio za jamii nchini Tanzania kwa lengo la kuwawezesha Watanzania walio wengi kupata elimu na hatimae kujinasua katika umaskini.
Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano la Mtandao wa Redio za Jamii katika nchi za Afrika Mashariki (EACOMNET) linalofanyika makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) mjini Arusha, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi mkazi wa UNESCO Zulmira Rodrigues alisema kwamba watu zaidi ya milioni 16 wengi wao wakiwa pembezoni mwa Tanzania wanategemea redio za jamii katika kuelimishwa masuala mbalimbali ya ustawi wa jamii jambo ambalo shirika lake linawajibika kwa redio hizo kwa kutoa misaada mbalimbali ili ziweze kujitegemea na kutoa huduma zake kikamilifu.
Alisema anaamini kwamba kwa miaka kadhaa ijayo redio za jamii zitakuwa chanzo cha maarifa kwa watu wengi nchini Tanzania kutokana na uasilia wake na kwa kuyatumikia maeneo ambayo kimawasiliano ni vigumu kufikika, na wakati huo huo vyombo vikuu vya mawasiliano kushindwa kukidhi mahitaji ya wanajamii jambo linalosababisha ukosefu wa kupata habari muhimu na kuzorotesha maendeleo katika jamii husika.
IMG_4942
Naibu Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Utawala na Fedha), Bw. Liberat Mfumukeko akisalimiana na Mwenyekiti wa Radio za Jamii kutoka UNESCO India, Prof. Vinod Pavarala katika chumba maalum cha wageni katika makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha.
Zulmira amezihimiza redio hizo kutoa huduma zinazostahili kwa jamii za kupasha, kuelimisha na kuburudisha, pamoja na kujiwekea mikakati wa kudumu ya kuhamasisha rasilimali fedha zitakazosaidia kuboresha huduma za redio na kuboresha mfumo wa mawasiliano kati kituo cha redio na wanajamii.
Miongoni mwa maboresho yatakayoendelezwa na Unesco ni kusaidia uhakiki wa ubora wa matangazo, vipindi vyenye kuzingatia maadili na ushirikishwaji wa makundi yote wakiwemo wanawake ,vijana ,watu wenye ulemavu na Albinism katika mchakato wa demokrasia, amani na maendeleo .
Kongamano hilo la siku tatu pamoja na mambo mengine linalenga kujadili namna ya kuziwezesha redio hizo kujiendesha katika mipango endelevu kwa kuwa na mipango sahihi ya kifedha bila kutegemea misaada kutoka kwa wafadhili ili ziweze kutoa mchango unaokusudiwa kwa wananchi.
Kwa niaba ya mtandao wa redio jamii ukanda wa Afrika Mashariki, mwenyekiti wa Mtandao wa redio za Jamii Tanzania, COMNETA Joseph Sekiku aliishukuru Unesco kwa kuziwezesha redio za jamii kutoka nchi za Afrika Mashariki kukutana kwa lengo kushirikiana na kupeana maarifa kuhusu uendeshaji wa redio hizo na zitakavyoweza kutekeleza kwa ubora malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu na UNESCO India kwa kuleta maarifa mapya kuhusu uendeshaji wa redio za jamii.
IMG_4980
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Utawala na Fedha), Bw. Liberat Mfumukeko katika chumba maalum cha wageni kabla ya kuelekea kwenye ufunguzi wa kongamano la siku tatu la Mtandao wa Redio za Jamii katika nchi za Afrika Mashariki (EACOMNET) linalofanyika makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha.
Nchi zilizoshiriki katika kongamano hilo ni Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda chini ya mwamvuli wa Mtandao wa Redio za jamii Afrika mashariki (EACOMNET), ukiwa na redio wanachama 50 zenye uwezo wa kuwafikia wasikilizaji milioni 35 kati ya watu milioni 120 waliomo katika nchi hizo.
Naibu Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Utawala na Fedha), Liberat Mfumukeko ameelezea kufurahishwa kwake kufanyika kwa kongamano hilo ambalo litasaidia redio jamii kupata maarifa zaidi na elimu kuhusu mtengamano wa Afrika Mashariki na kuufanikisha.
Alisema Jumuiya ya Afrika Mashariki inaelewa umuhimu wa vyombo vya habari hasa vya jamii kutokana na kazi yake kwa kuzingatia juhudi utekelezaji wake wa kuhamasisha jamii kuendeleza mtengamano wa Afrika Mashariki.
IMG_5030
Mwenyekiti wa Mtandao wa redio za Jamii Tanzania, (COMNETA), Joseph Sekiku akizungumza kwa niaba ya mtandao wa redio jamii ukanda wa Afrika Mashariki (EACOMNET) kabla ya kumkaribisha Prof. Vinod Pavarala.
IMG_5097
Mwenyekiti wa Radio za Jamii kutoka UNESCO India, Prof. Vinod Pavarala akieleza dhumuni na lengo la kongamano hilo kwa washiriki. Kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la UNESCO nchini, Zulmira Rodrigues.
IMG_5199
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Utawala na Fedha), Bw. Liberat Mfumukeko kufungua rasmi kongamano hilo linaloendelea jijini Arusha.
IMG_5266
Naibu Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Utawala na Fedha), Bw. Liberat Mfumukeko akifungua rasmi kongamano la siku tatu la Mtandao wa Redio za Jamii katika nchi za Afrika Mashariki (EACOMNET) linalolenga kujadili namna ya kuziwezesha redio hizo kujiendesha katika mipango endelevu kwa kuwa na mipango sahihi ya kifedha bila kutegemea fedha kutoka kwa wafadhili ili ziweze kutoa mchango unaokusudiwa kwa wananchi linaloendelea katika makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha.
IMG_5151
Mwenyekiti wa Radio za Jamii kutoka UNESCO, Prof. Vinod Pavarala akimkabidhi Ofisa Miradi katika kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph zawadi kwa heshima ya ukumbusho wa India.
IMG_5155
Ofisa Miradi katika kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akitoa shukrani zake kwa Prof. Vinod baada ya kupokea zawadi.
IMG_5060
Ofisa miradi mpya katika kitengo cha Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy Kaizilege akijitambulisha kwa hadhira ya washiriki wa kongamano.
IMG_5010
Sehemu ya washiriki katika kongamano hilo.
IMG_5382
Mhadhiri wa Chuo cha Uandishi wa Habari cha Hyderabad India, Dkt. Kanchan Malik akiongoza kikundi kazi kilichojumuisha washiriki kutoka Rwanda na Uganda.
IMG_5360
Mwenyekiti vyombo vya Habari Jamii kutoka UNESCO India, Prof. Vinod (aliyeipa mgongo camera) akiongoza kikundi kazi kinachojumuisha washiriki kutoka Burundi na Tanzania.
IMG_5281
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akifurahi jambo na Mjumbe wa bodi udhamini ya Mtandao wa Radio Jamii Tanzania (COMNETA), Balozi Mstaafu, Christopher Liundi nje ya chumba cha mikutano makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha.
IMG_5296
Mjumbe wa bodi udhamini ya Mtandao wa Radio Jamii Tanzania (COMNETA), Balozi Mstaafu, Christopher Liundi (kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Utawala na Fedha), Bw. Liberat Mfumukeko wakati wakielekea kwenye zoezi la picha ya pamoja.
IMG_5307
Picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa kongamano hilo.
IMG_5309
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akiwapungia kama ishara ya kuagana na washiriki wa kongamano hilo wakati akiondoka makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha kuanza safari ya kuelekea uwanja wa ndege tayari kurejea Dar es Salaam.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment