Ajali ya Mkurugenzi wa kituo cha LHRC, Dr. Hellen Kijo Bisimba yaibua maswali mitandao ya kijamii

10989453_856894261097306_3195698131161374537_o
Picha ya ajali hiyo kama inavyoonekana (Picha kwa hisani ya mitandao ya kijamii).
[DAR ES SALAAM-TANZANIA]  Saa chache zilizopita imetokea ajali mbaya inayoelezwa kuwa mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC.Dr. Hellen Kijo Bisimba amekumbwa na ajali hiyo  na  kukimbizwa Hospital kwa matibabu zaidi.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari ikiwemo mtandao wa habari wa Jamiiforum (JF) umechapisha taarifa hiyo pamoja na picha na kueleza  kuwa  ajali imetokea Barabara ya Ali Hassan Mwinyi Jijini Dar es salaam.
Hata hivyo mtandao huu umeweza kushuhudia maoni mbalimbali ya wananchi kupitia mitandao ya kijamii wakiibua maswali tofauti yasiyo na majibu huku wengine wakielezea ajali hiyo ni ya kawaida kama ajali zingine.
Miongoni mwa maswali hayo ni pamoja na kuwa wapo waliolieleza kuwa huenda kuna kitu nyuma ya pazia na wengine wakielezea kuwa ni mipango tu ya watu fulanifulani ambao wamekuwa wakichukizwa na msimamo wa harakati zake hapa nchini.
unnamed (9)
unnamed (8)
Gari hilo linavyoonekana 
NB: taarifa hii imetoka katika vyanzo vya habari ikiwemo mitanda ya kijamii ya facebook, twitter na whatsapp, Pia kama una habari na picha za matukio unaweza kutuma kwetu kupitia  Whatsapp +447557304940

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment