BAND YA SKYLIGHT KUENDELEA KUWAKONGA NYOYO MASHABIKI WAKE LEO NDANI YA ESCAPE ONE MIKOCHENI

Sony Masamba akiongoza marapa wenzake wa Skylight Band, Suzy (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Bijal Valentine(wa pili kutoka kushoto), Leah  pamoja na Kasongo Junior (kulia) wakiendelea kutoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Jumapili iliyopita ndani ya kiota cha Escape One Mikocheni ambapo leo pia burudani iko pale pale na ndio kwanza weekend imeanza kwa fans wa Skylight Band.

Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiimba huku akisindikizwa na wasanii wenzake.
 Suzy (wa pili kulia) akiongoza waimbaji wenzake wa Skylight Band,  huku akisindikizwa na Bijal Valentine(wa kwanza kushoto), Kasongo Junior  pamoja na Leah  (kulia) 
Waimbaji wa Bandi ya Skylight wakiongozwa na Leah(wa kwanza kulia) akiimba moja ya nyimbo zinazobamba hapa nchini Tanzania na hata nje ya nchi huku akisindikizwa na wasanii wenzake Suzy pamoja na Kasongo Junior  wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) ndani ya kiota cha Escape One jumapili iliyopita sasa leo sio siku ya kukosa njoo ujionee mambo mapya kutoka kwenye bandi ya Skylight
Sam Mapenzi wa Skylight band akiimba kwa hisia kali mbele ya mashabiki i wa bendi hiyo (hawapo pichani) waliofika kwenye kiota cha Escape One Mikocheni.

Bendi ya waimbaji wakali wa Skylight ikirindimisha baadhi ya nyimbo zao ndani ya kiota cha Escape One hii ni kwa kila jumapili njoo wewe na yule upate muziki mtamu kutoka kwenye bandi hiyo
Burudani ikiendelea kwenye kiota Escape One hakika wewe sio mtu wa kuikosa shoo za kila siku ya jumapili njoo upate muziki mzuri kutoka kwenye bendi ya wastaarabu
Kifaa kipya kutoka Bandi ya Skylight, Bijal Valentine akishusha mistari ya kufa mtu mbele ya mashabiki wao waliofika kwenye kiota Cha Escape One huku akisindikizwa na waimbaji wenzake kushoto ni Leah na kulia ni Suzy
Ni mwendo wa kuzirudi maana ndani ya Skylight ni burudani mwanzo mwisho
Sony Masamba ambaye ni mmoja wa waimbaji wa Skylight akiendelea kutoa burudani akisindikizwa na waimbaji wenzake katika kiota cha Escape One Mikocheni.
Mwimbaji wa Bendi ya Skylight, Kasongo Junior (kulia) akiimba sambamba na Suzy mbele ya mashabiki wao (hawapo pichani ) ndani ya Kiota cha Escape One jijini Dar
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment