IBADA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU GODFREY MNGODO, COLUMBUS, OHIO

Pr. Mwakabonga akiongoza ibada ya kumbukumbu ya marehemu Godfrey Mbiu Mngodo iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 31, 2015 Columbus, Ohio nchini Marekani na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo wafanyakazi wa kituo cha utangazaji Sauti ya Amerika idhaa ya Kiswahili (VOA). Marehemu Godfrey Mbiu Mngodo aliaga Dunia Tarehe 11 Septemba, 2015 Dar es Salaam na kuzikwa Tanga. Godfrey Mbiu Mngodo amefanya kazi katika sehemu mbalimbali kama Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), Voice of America, wizarani na kituo cha Channel Ten ameacha watoto 10 na wajukuu 14. PICHA NA KWANZA PRODUCTION/VIJIMAMBO
Mmoja ya mtoto wa marehemu Michael Mngodo akiwa na mwanae Alvin wakifuatilia ibada ya kumbukumbu ya mpendwa baba yake marehemu Godfrey Mbiu Mngodo iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 31, 2015 Columbus, Ohio nchini Marekani.
Familia ya Mngodo ikifuatilia Ibada.
Pr. Mwakaboma akifanya maombi kwa wanafamilia.
Michael Mngodo akisoma wasifu wa mpendwa baba yake. Kulia ni mtoto wake Alvin.
Ndugu, jamaa na marafiki wakifuatilia ibada. Kwa Picha zaidi bofya HAPA
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment