KAMPUNI YA STAR MEDIA TANZANIA LIMITED YASHINDA TUZO YA UBORA YA WQC

 Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na tuzo ya utoaji huduma bora waliyoipokea nchini Ufaransa mwishoni mwa mwezi Oktoba kutoka kwa kampuni ya Business Initiative Directions (BID). Pamoja naye kulia ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes, Bw. Lanfang Liao.
 Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akisisitiza jambo katika mkutano huo na wanahabari.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes, Bw. Lanfang Liao akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na tuzo ya utoaji huduma bora waliyoipokea nchini Ufaransa mwishoni mwa mwezi Oktoba kutoka kwa kampuni ya Business Initiative Directions (BID).


Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya Business Initiative Directions (BID) ya nchini Ufaransa imeitunuku kampuni ya StarTimes kutoka nchini tanzania tuzo ya World Quality Commitment (WQC) kwa utoaji huduma bora kwa wateja wake.

Sherehe za tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya 29 ziliyofanyika jijini Paris ambapo makampuni mbalimbali yalishinda yalishiriki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kuonyesha tuzo hiyo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao amesema kuwa hiyo ni habari njema si tu kwa kampuni bali kwa taifa kwa ujumla kwa utoaji wa huduma bora kwa wateja wake.

“Tuzo hii imetolewa jijini Paris, Ufaransa mwishoni mwa mwezi Oktoba ambapo kampuni ya Business Initiative Directions (BID) ndio waandaaji wakuu wa tuzo hizi ambazo zimefanyika mara ya 29 kwa mwaka huu.” Alisema Bw. Liao

“Utolewaji wa tuzo huu ulihusisha marais, wakurugenzi, viongozi wa makampuni na wafanyabiashara kwa ujumla ambao walikuwa wanapendekeza majina ya kampuni inayostahili tuzo hiyo kutoka sehemu mbalimbali duniani.”
Katika upigaji huo wa kura ambao hufanyika kwa siri bila ya hata kampuni inayopigiwa kura kujua. Baada ya upigaji huo wa kura kampuni ya StarTimes ambayo ndiyo pekee kutoka nchini Tanzania kujinyakulia tuzo hiyo ya heshima.

“Kwa niaba ya kampuni ya StarTimes ningependa kuchukua fursa hii kwanza kabisa kuwatangazia wateja wetu na watanzania kwa ujumla kuwa wao ndio sababu kubwa mpaka sisi kutunukiwa tuzo hii. Pili, ningependa watanzania wafahamu kuwa ushindi wa tuzo hii sio wa kampuni pekee bali ni kwa Tanzania kwa ujumla kwani StarTimes ndio kampuni pekee iliyotunukiwa tuzo hii.” Aliendelea bosi huyo

“Hivyo basi, ningependa kuwashukuru wateja wetu lakini kikubwa zaidi ni serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa kampuni zinazokuja kuwekeza nchini kuwahudumia wananchi wake. Tunawashukuru wadau kama vile Tanzania Investment Center (TIC), TCRA, na wizara zote bila ya kusahau vyombo vya habari ambavyo tumekuwa navyo bega kwa bega katika shughuli zetu.” Aliongezea

“Ni kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji nchi na wananchi wake wananufaika na kusonga mbele kimaendeleo.”

“Kwa kuhitimisha, ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru tena watanzania kwa kuendelea kutuamini na kutuunga mkono katika shughuli zetu na wakae mkao wa kula kwa kampeni zetu kabambe zinazoendelea kuzinduliwa hivi karibuni.” Alihitimisha


Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment