Msanii Bobo Seretsane "Bo" wa Afrika kusini afagilia muziki wa Tanzania, apongeza tamasha Karibu Music!

DSC_0896
Msanii nyota wa Afrika Kusini, Bo Denim "Bo" akitumbuiza jukwaani wakati wa tamasha la msimu wa pili la Karibu Music Festival..!
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[BAGAMOYO-TANZANIA] Mwanamuziki nyota kutoka Afrika Kusini Bo Denim maarufu ‘Bo’ amewashukuru waandaji wa tamasha la Music Festival linalofanyika kila mwaka mjini hapa huku likihusisha vikundi na wanamuziki mbalimbali kutoka mataifaa tofauti ya Afrika nan je ya Afrikaa.
Bo ambaye usiku wa jana Novemba 7, aliweza kupiga shoo hiyo kwa kiwango cha Kimataifa, alipata shangwe kwa mashabiki waliofurika kushuhudia tamasha hilo mjini hapa.
Baada ya shoo hiyo Modewji ilipata kufanya naye mahojiano ambapo amepongeza muziki wa Tanzania wakiwemo wasanii wanaovuma nje ya mipaka ya Tanzania. “Wasanii wa Tanzania wanauwezo mkubwa. Nimeshuhudia kundi la Weusi wamefanya vizuri sana” ameeleza Bo.
Tamasha hilo ambalo leo Novemba 8.2015, linatarajiwa kufikia tamati, linaratibiwa na Karibu Cultural Promotions Organization (KCPO) na Legendary Music Entertainment and Promotions Co. Ltd, T kwa kushirikiana na kampuni ya kinywaji cha Jebel Coconut. Wadhaminiwa wengine ni pamoja na Swiss Embassy, Precision Air, Coca Cola, Mwananchi Communication, Kaya fm, Magic fm, Focus Outdoor, Jovago, Kaymu na Time tickets.
DSC_0882
DSC_0858
DSC_0848
DSC_0843
DSC_0835
Bo akipagawisha mashabiki ...
DSC_0852
DSC_0884
DSC_0890
Mambo yalikuwa hivi ..
DSC_0884
DSC_0910
Host wa Karibu Music Festival 2015, Jazzphaa Nassor na Lulu wakishoo love wakati wa shoo hiyo ya "Bo"..
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment